2013 ni mwaka wa kubadili fikra zetu,na kusimamia usahihi,haki na wajibu.Tunuie toka ndani yetu,kuleta mabadiliko katika taifa hili.Wakati wa kuzubaa umeisha,wakati wa kulalamika umeisha,hatuna tena muda wa kuogopa.Kama kila kijana atatambua na kutimiza wajibu wake,tuwe na uhakika tutapata jamii ya vijana wanaowajibika,wanaowajibika kwa kumfuata Mungu,wanaowajibika katika familia zao,wanaowajibika katika masuala ya maendeleo ya taifa hili.UJANA NI FIKRA MAKINI,AMUA KUWA NA FIKRA MAKINI UWE KIJANA.
Sunday, December 23, 2012
Thursday, December 13, 2012
WATOTO WADOGO WAKIFIKIA UMRI KAMA WETU WA KUITWA VIJANA,WAONE NINI KATIKA TAIFA HILI?
Vijana wanakumbwa na changamoto
nyingi za kimaisha,taifa letu halina mpango rasmi na mfumo unaotambulika wa
kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za dunia yenye utandawazi,ubepari
ulio komaa,teknolojia inayokua kila kukicha.
Matokeo yake tumekuwa na kundi
kubwa la vijana waliokata tama na wasio wathubutu katika masuala ya
msingi,mamia ya vijana huko vijijini wanateseka na hali ngumu ya maisha,mamia
ya vijana hapa jijini Dar wameathirika na madawa ya kulevya,mamia ya vijana
wamekosa kutambua nini haswa maono ya taifa hili,mamia ya vijana wamebaki
wakilalamika huku na huko.Mamia ya vijana wameshindwa kutambua maana halisi ya
kuwa kijana.Twaenda wapi?
Hatuwezi kuvumilia hali hiyo,tuna
taka hawa watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa kuitwa vijana,waone nini
katika taifa hili?waone na kusikia yale ambayo mimi na wewe tumeyaona na
kuyasikia?Tunataka wapite njia tunayoipitia leo hii?
Mimi na wewe tupo hapa leo
hii,ili tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa
hili,hawa watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na
imara,itakayowawezesha wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa
ujana,kisha wakasema taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana
na changamoto za kimaisha.
Natoa wito kwa vijana wenzangu,wenye
uwezo,wenye maono na tunaolitakia mema taifa hili, kuanzisha miradi itakayogusa
watoto wa Tanzania,kwa ajili ya Tanzania ya kesho,vinginevyo tutakuwa tuna
twanga maji kwenye kinu.
Nina jitafakari makosa yangu ya
kimpango mkakati 2012, kwa ajili ya mpango mkakati 2013, wewe je?
Mungu wabariki vijana wa Tanzania
Mungu ibariki Tanzania.
na Baraka Daniel Kiranga(22)
+255762362413
baraka1990@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)