Mwaka 2011,nilipata kufuatilia kwa
ukaribu kuhusu mitandao ya kijamii.Nilipata muda wa kuchambua mtandao mmoja
baada ya mwingine,nilipaswa kufanya hivyo ili kubaini ni nani ni gwiji kati ya
mitandao hiyo.Nilipata kujua tofauti kati ya mtandao mmoja na mwingine,na
kwanini mtu utumie mtandao huu na usitumie mwingine.Na mwisho wa siku nilikuja
kutambua ya kwamba Facebook ndiyo ulikuwa mtandao uliotengenezwa kwa ubunifu wa
hali ya juu,na unaotoa huduma nyingi zaidi ukifana nisha na mitadano mingine,kama
twitter, linked in ,my space na mitandao mingineyo.Uchunguzi huo ulinichukua
muda,takribani mwezi mmoja. Kazi hii ilikuwa ni assignment yangu kwenye somo la
Business information systems,nilipaswa kutafuta kampuni moja na kuifananisha na
makampuni mengine,ili nipate kujua ninani kati yao ana competitive
advantage.Uchaguzi wangu ulidondokea kwenye social
networks.
Matumizi ya mitandao ya kijamii yamebadili maisha ya watu wengi sana,haswa namna ya upashanaji habari.Taarifa
zimekuwa zikiwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi,na vyanzo vya habari
vimeongezeka,ukilinganisha na miaka ya nyuma,na hii ni changamoto kwa TCRA
katika kudhibiti ubora na ukweli wa habari zinazowafikia mamia ya watu.
Kuongezeka kwa watumiaji wa mitandao
ya kijamii,ni ishara tosha ya kwamba watanzania walio na uelewa juu ya matumizi
ya internet unaongezeka,ni jambo jema hilo,ingawa tunapaswa kujiuliza maswali
ya msingi,je watumiaji wa internet wanatumia kwa usahihi,na je tunatumia viwango(standards) vipi kuamua ya kwamba mtu
huyu anatumia kwa usahihi na huyu hatumii kwa usahihi.Hayo yote tunapaswa
kutafakari na kuchukua hatua.
Watumiaji wengi wa mitandao ya
kijamii ni vijana na wengi wao hutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya
kuchat,kupost picha ambazo hazina mantiki na nyingi ni picha ambazo zimekosa
maadali. kitu ambacho kinawapotezea muda mwingi,na kuharibu fikra zao na
kupunguza uwezo wao wa kujikita katika masuala ya msingi,matokeo yake tumekuwa
na vijana wengi ambao hawajikita katika kujiletea maendeleo yao binafsi. Kuna
fursa nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii,iwapo tu mtumiaji ataamua kutumia
mitandao ya kijamii kama sehemu ya kujitengenezea fursa.
Na ni wito wangu kwa vijana kutumia
mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujitengenezea fursa za maendeleo
yao.Tusipoteze muda kwenye masuala ambayo si ya msingi pindi tunapokuwa
internert bali tutumie muda wetu kwenye kujifunza na kudadisi masuala ya msingi
yanayoweza kutufanya tuanze kujiletea maendeleo.
Makala
hii imeandikwa
na Baraka Daniel Kiranga(23)
0762362413
www.barakadaniel.blogspot.com
0 maoni:
Post a Comment