Saturday, March 24, 2012

USIFUGE MATATIZO, USIYAKUZE MATATIZO, USIKATE TAMAA.


Katika maisha yetu ya kila siku,tuna kutana na watu tofauti,tunaona vitu tofauti,tunasikia taarifa tofauti.Pia tuna kutana na matatizo na changa moto tofauti,baina ya mtu mmoja na mwingine.hatufanani tunavyokabiliana,na kutatua matatizo hayo pamoja na changamoto za maisha.tatizo linaweza likawa moja,lakini tukatofautiana jinsi ya kulitatua,kila mmoja na njia yake na mtindo wake wa kulishughulikia.

Utofauti huo utokea kwasababu tumepishana uwezo wa kufikiria baina ya mtu mmoja na mwingine(thinking capacity).Achilia mbali utofauti huo,sote kwa pamoja hujiuliza na kujihoji maswali mengi,pindi tunapokuwa katika matatizo.

Tunapokumbwa na matatizo makubwa huwa tuna dhani,hakuna watu wengine walio wahi kukumbwa na yanayotukumba,na huwa tuna kuwa na maswali mengi kweli kuliko majibu,wapo ambao huwa wanakata tama ya kuishi na wanaamua kujinyonga,wapo wanaochanganyikiwa na hatimaye kuwa vichaa,wapo wanaozidisha juhudi katika kutafuta majibu zaidi na zaidi huku wakimwamini na kumuomba Mungu-watu wa namna hii ni wachache sana,wapo wanowaza na kuona matatizo waliyo nayo yanasababishwa na mtu au watu fulani hivyo muda mwingi huwalalamikia hao wanaodhani kuwa ndiyo chanzo cha matatizo yao,wapo wanaopindukia na kudumbukia katika dimbwi la ulevi wakidhani ya kwamba watakapotoka dimbwini watakuta matatizo yamepotea kusikojulika pasipo kutambua ya kwamba wanajiongezea matatizo.

Sote tuna matatizo.

Watu wote duniani,Wanawake kwa wanaume,weupe kwa weusi na ,wanene kwa wembamba,warefu kwa wafupi,matajiri kwa maskini,wanene kwa wembamba,wasomi na wasio wasomi,wenye vyeo na wasio na vyeo,wenye umaarufu na wasio na umaarufu.Sote kwa pamoja tunakumbwa na matatizo,unaweza ukadhani jamii ya watu fulani( mfano,matajiri)haina matatizo,lakini ukichunguza kwa undani utagundua nao pia wana matatizo yao,unaweza ukadhani ya kwamba unaumwa sana,kama una uwezo wa kutembea nenda hospitali ukaone watu wanavyoumwa na wanavyoteseka usiku na mchana,wanavyoshindwa kula,nakwambia ghafla utajiona wewe huumwi.

Unaweza ukaona una tatizo la pesa,lakini tambua kuna mtu hana fedha ata hizo ulizonazo wewe na wala hajui atazipataje.Kupata hasara ni kitu kibaya,wala hakuna anayependa kupata hasara,unaweza ukapata hasara ya milioni tatu au ata kumi,lakini tambua kuna watu hapa duniani washa wahi kupata hasara ya mabilioni ya fedha,na wala hawakukata tamaa katika biashara zao,huna haja ya kukata tamaa.

Inawezekana umewahi fungwa jela miaka mitatu au ata minne,au ndugu yako yupo jela na huu ni mwaka wa sita au saba,Hebu kumbuka Mzee Madiba(Nelson Mandela) alivyokaa gerezani miaka 27,na akatoka na bado akawa raisi wa Afrika kusini.

Yawezekana masomo kwako ni magumu sana,na inachukua muda kuelewa,ya wezekana rafiki yako mpendwa amekuumiza sana,yawezekana umeonewa,umeibiwa,umenyanyaswa,umefeli,hujui la kufanya,mwaka wa tatu huu tangu umalize chuo kikuu na bado hujapata ajiri rasmi.yawezekana watu wote wanakuona wewe unamakosa mengi sana,tambua moja tu “MUNGU YUPO UPANDE WAKO,USIKATE TAMAA”

Matatizo,hayamaanishi kwamba huo ndiyo mwisho wako wa maisha.

Kuna watu ,wamefika mahali wanaona matatizo waliyonayo ni sehemu ya maisha yao,na hivyo matatizo waliyo nayo hawayaoni kama ni matatizo,bali ndivyo maisha yalivyo na wamefika mahali wanaamini binadamu wengine wanaishi maisha kama yao.Lakini hiyo si kweli.

Tambua nyakati ngumu hazidumu kwa muda mrefu maishani.Hukuja duniani kwa bahati mbaya,ulikuja kwa makusudi maalumu,yawezekana kuna watu wanakudharau na wanakuona wewe si kitu,isikupe shida sana,Mungu aliyekuumba anakuona wewe ni wathamani sana na ndiyo maana mpaka sasa amekupa uhai na anakupenda sana,upendo wake hauwezi ukualinganishwa na upendo wa wanadamu,upendo wake ni mkuu mno,unapokumbwa na matatizo yeye ndiye jibu lako,utakapokimbiwa na watu yeye hatakukimbia,yupo pamoja nawe siku zote za maisha yako.Matatizo yana kuja na kuondoka,wewe utabaki na kuendelea na maisha(problems comes and go, but you’re here to stay)

Ukianguka nyanyuka,ukishindwa omba unyanyuliwe.

Ukipatwa na tatizo,fikiri kiundani,hakuna muda tunapaswa kufikiri kiundani na kuwa na umakini kama kipindi tunapokuwa na matatizo.ukiona unashindwa kupata jibu au suluhu ya matatizo yako,usikae kimya na tatizo linalokukabili,namaanisha usifuge matatizo,mifugo ndiyo inayofugwa mpendwa wangu,tupo pamoja rafiki,tafuta mtu unayemuona ana busara na unamfahamu kiundani,muombe ushauri juu ya kutatua tatizo linalokukabili,omba ushauri kwa watu waliofanikiwa katika maisha,utagundua wao walipitia magumu zaidi yako,usiwe na haraka ya kutatua tatizo,kuwa mstaarabu na mwenye adabu,hebu angalia tu,siku zote simba anapokuwa mawindoni anakuwa mtaratibu sana,mwenye nidhamu(displine) ya hali ya juu,anapiga hatua za miguu yake kwa umakini wa hali ya juu,kimya kimya,akiendea windo lake,mpaka anafanikiwa kupata chakula chake.Wewe ni binadamu unaakili sana na utashi,kuliko kiumbe kingine chochote,onyesha akili zako na utashi wako unapokabiliana na matatizo.

Tatizo linapokuwa fursa

Mtu mwenye malaria,kama hajapima na kugundulika ana malaria,anaweza akadhani tatizo alilonalo ni maaumivu ya kichwa tu,taratibu utamuona akinywa dawa ya kutuliza maumivu ya kichwa,akidhani ametatua tatizo,baadaye tena kichwa kinaanza kumuuma,anakunywa tena dawa,pasipo kutambua anatibu dalili ya tatizo na siyo tatizo,akiona amezidiwa ndiyo utamuona anakwenda kumuona daktari,baada ya kumuona daktari,na kupimwa,bila shaka,daktari atamwambia unasumbuliwa na malaria,na siyo kichwa,tumia dawa hizi utapona malaria.Wewe je,tatizo ulilonalo ni tatizo,au ni dalili ya tatizo haswa,je unajua kiini cha tatizo lako(problem’s root),kutambua kiini cha tatizo unaitajika,upate mahali tulivu na ufikiri kwa umakini na kwa ufasaha juu ya tatizo haswa nini?sijakwambia ulikuze tatizo,nimekwambia hivi tambua kiini cha tatizo,ukijua mzizi,na ukiuona utaungo’a pasipo kutumia nguvu nyingi.watu wengi tuna tumia nguvu kubwa sana,kwenye vitu ambavyo havikustahili kutumia nguvu,na tumepoteza muda mwingi sana hapo.

Nikwambie kitu rafiki?nuwia kubadilika unavyo ya tazama matatizo,mimi na kwambia ukikaa vizuri na ukituliza akili utaona matatizo ni fursa,hebu fikiria,mtu mwingine anaona ni tatizo kuingia mgodini ilihali mwingine anaona kuingia mgodini ni fursa ya yeye kupata fedha,mtu wa namna hii analiona shimo la kuingilia mgodini kama mlango wa fursa,na anamshangaa anayeona mgodi ni tatizo.Lifanye tatizo lako liwe fursa.Najua tumeelewana rafiki yangu ninayekupenda.

Hatua za kutambua kiini cha Tatizo.

1.Andika unavyojisikia unapokuwa katika matatizo(mfano,unachukia kupita kiasi,kujiona hufai, n.k)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

2. unadhani kwanini hali hiyo inakutokea/sababu ya hisia unazokuwa nazo katika kipindi cha matatizo(mfano,mtu anayenisababishia tatizo mara nyingi huwa ninakuwa naye pamoja,kwa sababu sipate fedha niliyoikusudia kuipata,kwa sababu ninasemwa vibaya n.k.)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

3.Unapotambua kinachokusababishia hisia mbaya wakati wa matatizo,huwa una chukua hatua gani?(mfano,nalia sana,nakunywa pombe,sielewi cha kufanya,namfokea yeyote anayekuwa mbele yangu,sitaki kumuona mtu yeyote,)

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

4.hatua unazochukua uwa zina kusaidia kwa kiasi gani?huwa zinaondoa tatizo moja kwa moja pasipo kujirudia tena,au zina kutuliza tu(temporary solutions)?

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

5.Nani huwa unamweleza shida zako?ni mtu aliye na uwezo wa kututatua matatizo,au unasema tu ili upunguze kama sio kuondoa hisia zako,maana usije ukawa unawanufaisha wengine na wakaishia kukukejeli?

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

6.Kabla ya kukumbwa na tatizo,je huwa unatafuta majibu ya matatizo yanayoweza kukumba kwa baadaye.mfano kama unaenda ugenini ni lazima uhakikishe unachaji simu yako kabla ya kuanza safari,ili tu uepushe tatizo la kupoteza mawasiliano na wenyeji wako.Jifunze kujipanga kutatua matatizo,kabla hayajatokea.Wewe huwa unafanya nini kabla ya kukumbwa na tatizo.

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

8.Je mfumo wako wa maisha na tabia yako,ndiyo chanzo cha matatizo yako?

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

Mpaka hapa najua utakuwa umeshagundua,nini haswa ni tatizo lako,siyo hisia,wala watu,wala huna sababu ya kumchukia mtu yeyote,kama unachuki na mtu yeyote,achana nahizo hisia za chuki hazitakusaidia zaidi zaid zitakuumiza wewe,wala ata unayemchukia hana habari,waswmehe watu,wapende watu,wathamini watu.Tambua ni wewe mwenyewe umeliona tatizo kama kikwazo kwako,namaanisha fikra zako.

badili fikra zako,ili uanze kuona fursa na siyo matatizo,badili mfumo wako wa maisha, hakikisha unakuwa na msimamo madhubuti.

Huu ni wakati wa kubadili fikra zetu,na kusimamia usahihi,haki na wajibu.Tunuie toka ndani yetu,kuleta mabadiliko katika maisha yetu.Wakati wa kuzubaa umeisha,wakati wa kulalamika umeisha,hatuna tena muda wa kuogopa.Kama kila kijana atatambua na kutimiza wajibu wake,tuwe na uhakika tutapata jamii ya vijana wanaowajibika,wanaowajibika kwa kumfuata Mungu,wanaowajibika katika familia zao,wanaowajibika katika masuala ya maendeleo ya taifa hili.

UJANA NI FIKRA MAKINI, AMUA KUWA NA FIKRA MAKINI UWE KIJANA.

Na; Baraka Daniel Kiranga.

+255762362413.

Makala hii ni moja kati ya makala zinazoandikwa na Baraka(miaka 21),ndoto yake nikuona vijana wa Tanzania,wakitumia uwezo wao(potentials, spiritual gifts, talents)walizopewa na Mungu,kwa manufaa yao wenyewe na kwa taifa zima na kuona Tanzania yenye mafanikio ifikapo 2040.( Baraka’s vision, is to see inspired great thinkers generation by 2040 in all corners of Tanzania, he wants to see every Tanzanian learn at least one inspiration book by 2040,when they will be inspired, they will inspire and we will have inspired Tanzania).Muunge mkono,kwa kuamua kusoma kitabu(inspiration book) walau kimoja,na tuma makala hii kwa rafiki yako.

0 maoni:

Post a Comment