Na Baraka
Daniel Kiranga(23).
Dar es
Salaam
Tanzania
Kuna
mambo mengi sana yanayotokea katika jamii yetu,na kila jambo lina sababu
yake,na maana yake pindi linapotokea katika maisha yetu.Sisi kama vijana hatuna
budi kujifunza katika hayo,tujifunze kutoka makosa ya kiungozi yanayotokea leo
hii,tujifunze kutoka makosa ya kiutendaji yanapotokea leo hii,tujifunze kutoka
matatizo ya kimaadili yanayozikumba nchi za Afrika ya mashariki na dunia kwa ujumla.
Kwa nini natoa wito wa kujifunza katika makosa ya liyofanywa na watu wengine? Jibu
pekee ni kutoruhusu matatizo hayo kujitokeze tena katika miaka ijayo, kwani
tutakuwa tumepata utashi wa kuyazuia yasitokee au kukabiliana nayo pindi
yanapotokea.Vijana tunapaswa kutambua ni sisi ndiyo tunaoamua mustakabali wa
maisha yetu.
Yanayotokea
leo hii,yana ashiria nini?yana ashiria ya kwamba Afrika Mashariki ipo kwenye
mpito(Transion period),kuna mahali
tunatoka na kuna mahali tuna kwenda,kuna mabadiliko ya kiuchumi yana yotokea
katika nchi zetu za Afrika mashariki,Kuna mabadiliko ya kisiasa na kiungozi
yanayotokea,kuna mabadiliko mengi yanatokea,katika hayo mabadiliko hatuna budi
kujifunza na kutafakari kwa undani ili tujue nini maana ya mabadiliko hayo,na
lipi tufanye kwa ajili ya mustakabali wa maisha yetu yajayo na vizazi vijavyo.
Tunapojifunza
na kutafakari tuna kuwa katika nafasi nzuri ya kujipanga kimkakati kwa ajili ya
kushughulika na matatizo sugu na masuala muhimu katika maendeleo ya watu wa
ukanda wa Afrika mashariki,na tunapo anza kuongelea maendeleo ya
watu,tunaongelea elimu yao,afya zao,miundo mbinu wanayotumia kila siku katika
shughuli zao za maendeleo.
Sisi
vijana leo tunajifunza yapi?Tungejibu vipi swali hilo kama tungeulizwa,au kila
mmoja angekuwa na majibu yake?Je tunajua historia ya nchi zetu kabla na baada
ya uhuru?Tunafahamu nini kuhusu uchumi wetu?nini haswa tuna itaji katika maisha
yetu?
Kama
kweli tuna taka uchumi wa nchi zetu ukue na kuwa uchumi imara,hatuna budi
kujifunza Zaidi masuala ya uchumi,na kuwa wathubutu kwenye shughuli za kiuchumi
na uzalishaji mali.Tukumbuke mustakabali wa Afrika Mashariki upo kwetu sisi
vijana,tunapaswa kujifunza,tunapaswa kuwa wabunifu,na watendaji kwa ajili yetu
na maendeleo ya nchi zetu.
Usipo
wajibika wewe,nani mwingine awajibike,chukua hatua.Mwaka 2014 tunuie kujifunza
na kutenda.