Friday, July 5, 2013

TANZANIA NA DIGITAL ECONOMY




Tunaishi katika dunia ambayo mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia ya naongezeka kwa kasi kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.Mifumo yote miwili (Uchumi na teknolojia) ndiyo inayopelekea watu wa jamii fulani wawe na mfumo wa aina fulani wa maisha. Kwa mfano jamii iliyo na uchumi imara,utoa uhakika wa upatikanaji wa ajira na huduma  muhimu katika jamii kama vile upatikanaji wa elimu,huduma za afya,miundo mbinu imara.

jamii yenye uchumi imara ni jamii yenye watu wenye afya njema,na maisha bora,na fikra zao huwa ni fikra zisizo na mawaa ya ajabu ajabu,na mara nyingi jamii zenye uchumi imara zina teknolojia ya hali ya juu,ukifananisha na jamii zenye uchumi ambao si imara.Mataifa ambayo uchumi wake umedorora hukumbwa Zaidi na matatizo ya ajira,Vijana wanapaswa kuelewa kwamba kinachotoa ajira si mfumo wa kisiasa,bali ni mfumo wa uchumi,mfumo ukiwa m’bovu basi ajira itakuwa ni tatizo, bali uchumi ukiwa imara tatizo la ajira litakuwepo kwa kiasi kidogo.

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano “Information Technology” katika miaka ya hivi karibuni yamekuwa kwa kasi kubwa sana,na ata kubadili mfumo wa maisha ya kijamii baina ya mtu na mtu,mathalani mitandao ya kijamii(kama facebook,twitter,blogs)imepelekea kubadili mfumo wa upashanaji wa habari katika jamii.Leo hii mtu yeyote aliye na ufahamu wa kutumia internet,anaweza akawa chanzo cha habari(Source of information),na habari atakayo itoa ikawafikia maelfu ya watu ndani ya dakika chache sana.

Si tu kwamba teknolojia ya mawasiliano imebadilisha mfumo wa upashanaji wa habari,bali pia ata shughuli za kiuchumi.Siku za hivi karibuni tumekuwa mashahidi na kujionea mifumo ya mawasiliano “Information systems” ikifungwa katika taasisi mbalimbali “organizations”,leo si kitu cha ajabu, kwa benki kuwa na “information security system”, hospitali kuwa na “hospital management information system”,vyuo na shule kuwa na “students information system”, maduka makubwa kuwa na “store reservation system”.Hali hiyo imepelekea mfumo mzima wa utendaji kazi wa organizations hizo kubadilika kabisa na ata kupelekea mfumo wa uchumi wa taifa kubadilika.

Mataifa kama Marekani yameendelea sana katika technolojia ya mawasiliano.Teknolojia ya mawasiliano imekuwa si sehemu ya maisha bali ni maisha halisi ya kila siku,kuna baadhi ya maeneo ukienda katika mataifa ya wenzetu ukiwa na fedha cash,unaweza usinunue chochote kwani mfumo wa malipo umekuwa wa kidijitali sana “Pure digital payments systems”,yaani fedha zina amishwa tu kutoka akaunti moja kwenda nyingine,kulingana na manunuzi yaliyofanyika,pasipo mnunuzi kulipa moja kwa moja.
Tunakoelekea dunia nzima,inalazimishwa kuingia katika mfumo wa “digital economy”.Teknolojia ya mawasiliano ndiyo itakuwa nguzo mama wa mfumo huo wa uchumi,aliye na teknolia ya hali ya juu Zaidi ya mwenzake,ndiye atakaye kuwa na uchumi mzuri Zaidi ya mwenzake na kuwa kinara wa maendeleo,waswahili wana kwambia “Mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama”.Tukifia hatua hiyo shughuli zote za uchumi zitakuwa za kidijitali na zinazoendeshwa kwa mifumo ya kielekronia,na hivyo basi tutakuwa na mataifa yanayotegemea na kuendeshwa na  digital economy.
Mataifa makubwa,yalisha tuacha maili nyingi tu za kutosha katika mbio hizi za teknolojia ya mawasiliano.Taifa kama marekani lina makampuni mengi sana ya nayojihusisha teknolojia ya mawasiliano,mfano kama google, Facebook, Microsoft, apple.
Hakuna sababu ya kukata tamaa ata kama tumeachwa mbali sana, tunachopaswa kutambua maisha ni sasa na wakati wa kuamka ndiyo huu,leo kila mmoja wetu anapaswa aanze kujifunza kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa manufaa zaidi na kwa kujitengenezea fursa za kiuchumi,kijamii na ata kisiasa,moja ya sababu ya Obama kushinda uchaguzi wa marekani mwaka 2008,ni jinsi alivyoendesha kampeni yake kwa njia ya kidijitali “21st century campaign” kitu ambacho mpinzani wake John McCain hakufanya,kuna haja ya kujifunza kutumia internet kama chombo cha kujitengenezea fursa.Mfano mzuri hapa Tanzania ni mjengwablog.com,situ kwamba ni sehemu ya kupata habari bali imekuwa ni ajira kwa wale ambao wanaofanya kazi na Maggid  mjengwa.
Swala la msingi ni jamii nzima kuhamasishwa kuwa na matumizi ya teknolojia,katika njia ambayo ni sahihi zaidi na yenye manufaa kwa maisha yao na vizazi vyao vijavyo.Wanafunzi wanaosoma masomo ya teknolojia,wanapaswa kuumiza bongo zao,ili waibuke na ubunifu utakao tatua matatizo sugu katika taifa letu.
Jamii yetu ikihamasika na kuanza kutumia teknolojia katika shughuli za kiuchumi,tutakuwa na Tanzania inayotegemea uchumi wa kidijitali “digital economy”.Kufika huko inawezekana kabisa,lakini tunapaswa kutambua hatutafika huko ndani ya siku moja,mwezi mmoja,mwaka mmoja,bali itatuchukua miaka mingi sana kuwa taifa linalotegemea na kuendeshwa na digital economy.
kuwa sehemu ya mabadiliko unayotaka kuyaona Tanzania.
Mungu ibariki Tanzania

Makala hii imeandikwa
 na Baraka Daniel Kiranga(22)
0762362413
www.barakadaniel.blogspot.com







1 maoni:

Anonymous said...

tutafika tu hakuna matata...

Post a Comment