Thursday, March 20, 2014

UWE SAUTI YAO, KAMA ANNA AIDAN ALIVYO SAUTI YAO

Mwaka juzi 13/12/2012, Niliandika Makala yenye kichwa “watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa kuitwa vijana,waone nini katika taifa hili?”,Makala hii inapatikana katika blog yangu,kama iliyvo ada ya blog yangu kuandika juu ya masuala ya msingi na habari za kuhamasisha(inspiration),na siyo zile habari za nani alikuwa na nani “week end” liyopita,nani alipendeza Zaidi ya mwenzeka,nadhani tunapaswa kujadili masuala ya msingi Zaidi juu ya maisha yetu sisi vijana,taifa letu bado ni maskini ingawa halikupaswa kuwa taifa maskini,hatma ya taifa hili ipo mikononi mwetu.

Moja ya maneno yaliyopo katika makala ile ni “Mimi na wewe tupo hapa leo hii,ili tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa hili,hawa watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na imara,itakayowawezesha wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa ujana,kisha wakasema taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana na changamoto za kimaisha.”.

Na hapo ndipo nitakapo anzia leo hii. Tarehe 14/7/2013,mida ya sa nane mchana na dakika zake,nikiwa mitaa ya posta,jijini Dar es salaam,nilikutana na rafiki yangu.anaitwa Anna Aidan,tulisalimiana naye kwa furaha,Anna ni rafiki yangu wa karibu,sote tulikuwa tunaelekea njia moja,hivyo tulipanda gari moja,hakukuwa na foleni sana siku hiyo,kwani ilikuwa ni siku ya jumapili.
Kama ilivyo ada ya marafiki wanapokutana,wata peana habari za hapa na pale na kuulizana juu ya kila mmoja juu ya maisha yake,na mipango aliyo nayo.Katika mazungumzo yetu,tulijikuta tunajadili juu ya watoto wanao ishi mitaani na wanao omba omba, katika ya jiji.
Anna alinieleza jinsi anayoumizwa na hali hiyo ya kuona watoto wadogo wakiteseka na maisha ya kuomba omba na pasipo kuijua kesho yao na hatma ya maisha yao. Alinieleza ya kwamba kuna baadhi ya watoto wanaomba omba,na kiuhalisia hawapendi kuomba.Na akatoa mawazo yake ya kwamba serikali ilipaswa iwe na kituo maalumu cha kuwatunza watoto hao na kuwapatia malezi bora.
Sio kwamba serikali ndiyo inapaswa kuwa muasisi wa kuwatunza watoto hao,bali  kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuyaishi mabadiliko anayoyataka katika jamii.wakati tuna endelea na mazungumzo yetu,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimsaidia mototo mmoja ambaye anaomba mitaa ya posta,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimnunulia yule mototo chakula,na ata kuongea naye,ili apate kujua nini haswa chanzo cha yeye kuomba. Msaada wa Anna kwa huyo mototo hauishi hapo,lakini pia amefika mahali anampatia mtoto huyo fedha kwa ajili ya matibabu.
Na pindi mtoto huyo,anapopatiwa fedha,anakwenda hospitalini,na akirudi ana muonyesha Anna dawa alizopewa hospitalini.Anna ananimbia,mtoto huyo moja kwa moja inaonekana hana asili ya kuomba omba.
Kuna mamia ya watoto katika taifa letu,wanapitia maisha magumu na hakuna mtu wa kuwasikiliza,na wala hawajui nini maana ya upendo,na wanaona jamii imewatenga na wao siyo sehemu ya jamii.Kuna Ongezeko la watoto wa mitaani kadiri siku zinavyo songa mbele,na hakuna hatua madhubuti ambazo zimekuwa zikichukuliwa,na kiuhalisia hawapaswi kuitwa watoto wa mitaani,kwani mtaa haujawai kuzaa mtoto,kuna mtu kwenye jamii anakwepa wajibu wake,sitaki kuamini kabisa ya kwamba hao watoto wanakosa ndugu kabisa.

Anna,ameyaishi mabadiliko anayoyataka kuyaona katika taifa letu,na amekuwa sauti ya matumaini kwa huyo mtoto.Kuna somo la kujifunza hapa.Wewe ni nani katika jamii yetu?au unalalamika tu juu ya mambo yanavyokwenda kombo,mabadiliko hayatakuja kama wewe hutabadilika,MABADILIKO NI WEWE.