Mwaka juzi 13/12/2012,
Niliandika Makala yenye kichwa “watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa
kuitwa vijana,waone nini katika taifa hili?”,Makala hii inapatikana katika blog
yangu,kama iliyvo ada ya blog yangu kuandika juu ya masuala ya msingi na habari
za kuhamasisha(inspiration),na siyo zile habari za nani alikuwa na nani “week
end” liyopita,nani alipendeza Zaidi ya mwenzeka,nadhani tunapaswa kujadili
masuala ya msingi Zaidi juu ya maisha yetu sisi vijana,taifa letu bado ni
maskini ingawa halikupaswa kuwa taifa maskini,hatma ya taifa hili ipo mikononi
mwetu.
Moja
ya maneno yaliyopo katika makala ile ni “Mimi na wewe tupo hapa leo hii,ili
tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa hili,hawa
watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na imara,itakayowawezesha
wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa ujana,kisha wakasema
taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana na
changamoto za kimaisha.”.
Na
hapo ndipo nitakapo anzia leo hii. Tarehe 14/7/2013,mida ya sa nane mchana na
dakika zake,nikiwa mitaa ya posta,jijini Dar es salaam,nilikutana na rafiki
yangu.anaitwa Anna Aidan,tulisalimiana naye kwa furaha,Anna ni rafiki yangu wa
karibu,sote tulikuwa tunaelekea njia moja,hivyo tulipanda gari moja,hakukuwa na
foleni sana siku hiyo,kwani ilikuwa ni siku ya jumapili.
Kama
ilivyo ada ya marafiki wanapokutana,wata peana habari za hapa na pale na
kuulizana juu ya kila mmoja juu ya maisha yake,na mipango aliyo nayo.Katika
mazungumzo yetu,tulijikuta tunajadili juu ya watoto wanao ishi mitaani na wanao
omba omba, katika ya jiji.
Anna
alinieleza jinsi anayoumizwa na hali hiyo ya kuona watoto wadogo wakiteseka na
maisha ya kuomba omba na pasipo kuijua kesho yao na hatma ya maisha yao.
Alinieleza ya kwamba kuna baadhi ya watoto wanaomba omba,na kiuhalisia
hawapendi kuomba.Na akatoa mawazo yake ya kwamba serikali ilipaswa iwe na kituo
maalumu cha kuwatunza watoto hao na kuwapatia malezi bora.
Sio
kwamba serikali ndiyo inapaswa kuwa muasisi wa kuwatunza watoto hao,bali kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuyaishi
mabadiliko anayoyataka katika jamii.wakati tuna endelea na mazungumzo
yetu,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimsaidia mototo mmoja ambaye anaomba
mitaa ya posta,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimnunulia yule mototo
chakula,na ata kuongea naye,ili apate kujua nini haswa chanzo cha yeye kuomba.
Msaada wa Anna kwa huyo mototo hauishi hapo,lakini pia amefika mahali anampatia
mtoto huyo fedha kwa ajili ya matibabu.
Na
pindi mtoto huyo,anapopatiwa fedha,anakwenda hospitalini,na akirudi ana
muonyesha Anna dawa alizopewa hospitalini.Anna ananimbia,mtoto huyo moja kwa
moja inaonekana hana asili ya kuomba omba.
Kuna
mamia ya watoto katika taifa letu,wanapitia maisha magumu na hakuna mtu wa
kuwasikiliza,na wala hawajui nini maana ya upendo,na wanaona jamii imewatenga
na wao siyo sehemu ya jamii.Kuna Ongezeko la watoto wa mitaani kadiri siku
zinavyo songa mbele,na hakuna hatua madhubuti ambazo zimekuwa zikichukuliwa,na
kiuhalisia hawapaswi kuitwa watoto wa mitaani,kwani mtaa haujawai kuzaa
mtoto,kuna mtu kwenye jamii anakwepa wajibu wake,sitaki kuamini kabisa ya
kwamba hao watoto wanakosa ndugu kabisa.
Anna,ameyaishi
mabadiliko anayoyataka kuyaona katika taifa letu,na amekuwa sauti ya matumaini
kwa huyo mtoto.Kuna somo la kujifunza hapa.Wewe ni nani katika jamii yetu?au
unalalamika tu juu ya mambo yanavyokwenda kombo,mabadiliko hayatakuja kama wewe
hutabadilika,MABADILIKO NI WEWE.
0 maoni:
Post a Comment