Sunday, December 23, 2012

MWAKA 2013 NI MWAKA WA KUBADILI FIKRA ZETU

2013 ni mwaka wa kubadili fikra zetu,na kusimamia usahihi,haki na wajibu.Tunuie toka ndani yetu,kuleta mabadiliko katika taifa hili.Wakati wa kuzubaa umeisha,wakati wa kulalamika umeisha,hatuna tena muda wa kuogopa.Kama kila kijana atatambua na kutimiza wajibu wake,tuwe na uhakika tutapata jamii ya vijana wanaowajibika,wanaowajibika kwa kumfuata Mungu,wanaowajibika katika familia zao,wanaowajibika katika masuala ya maendeleo ya taifa hili.UJANA NI FIKRA MAKINI,AMUA KUWA NA FIKRA MAKINI UWE KIJANA.

Thursday, December 13, 2012

WATOTO WADOGO WAKIFIKIA UMRI KAMA WETU WA KUITWA VIJANA,WAONE NINI KATIKA TAIFA HILI?


Vijana wanakumbwa na changamoto nyingi za kimaisha,taifa letu halina mpango rasmi na mfumo unaotambulika wa kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za dunia yenye utandawazi,ubepari ulio komaa,teknolojia inayokua kila kukicha.

Matokeo yake tumekuwa na kundi kubwa la vijana waliokata tama na wasio wathubutu katika masuala ya msingi,mamia ya vijana huko vijijini wanateseka na hali ngumu ya maisha,mamia ya vijana hapa jijini Dar wameathirika na madawa ya kulevya,mamia ya vijana wamekosa kutambua nini haswa maono ya taifa hili,mamia ya vijana wamebaki wakilalamika huku na huko.Mamia ya vijana wameshindwa kutambua maana halisi ya kuwa kijana.Twaenda wapi?

Hatuwezi kuvumilia hali hiyo,tuna taka hawa watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa kuitwa vijana,waone nini katika taifa hili?waone na kusikia yale ambayo mimi na wewe tumeyaona na kuyasikia?Tunataka wapite njia tunayoipitia leo hii?

Mimi na wewe tupo hapa leo hii,ili tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa hili,hawa watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na imara,itakayowawezesha wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa ujana,kisha wakasema taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Natoa wito kwa vijana wenzangu,wenye uwezo,wenye maono na tunaolitakia mema taifa hili, kuanzisha miradi itakayogusa watoto wa Tanzania,kwa ajili ya Tanzania ya kesho,vinginevyo tutakuwa tuna twanga maji kwenye kinu.

Nina jitafakari makosa yangu ya kimpango mkakati 2012, kwa ajili ya mpango mkakati 2013, wewe je?

Mungu wabariki vijana wa Tanzania
Mungu ibariki Tanzania.

na Baraka Daniel Kiranga(22)
+255762362413
baraka1990@gmail.com

Friday, November 30, 2012

Realizing Your Dreams

You have a dream, so what’s next? How do you bring your dream to pass? What do you do when you hit insurmountable roadblocks? Like the captain of a ship in the midst of a brutal storm, Myles Monroe safely guides you through the rough waters to your port of destiny.

You were born to win and Dr. Monroe will inspire you to take your life out of neutral and get busy about fulfilling your God-given vision!












by Dr. Myles Monroe

I Have a Dream!
If you have a dream, or if you want to discover your vision, remember this: God loves dreamers. He gives visions, and He is attracted to people who love to dream big. Don’t forget that you are unique, special, and irreplaceable.

You are not meant to be like anyone else.

When you decide to be part of the norm, your destiny is shortchanged. God wants you to stir up the gift He has given you and to develop it to the fullest.

Take a Lesson From The Winners and Doers…
What is the difference between the dreamer who realizes his dream, and the dreamer whose dream becomes a nightmare of unfulfilled hopes?

The dreamer who succeeds is someone who has a clear vision and acts on it. As long as a person can hold on to his vision, then there is always a chance for him to move out of his present circumstances and toward the fulfillment of his purpose.

Living Your Life’s Vision!
If you feel trapped, underemployed, or underutilized in your job; if you own your own business and want it to grow; if you want to know how to pursue your goals in life; if you are the leader of an organization or group; if your children are grown or in school now, and you are considering reviving old interests, or wherever you are in life right now, my desire is that you will be inspired, motivated, and challenged to get back in the race toward your dream, to get back the passion toward your goal.

I want you to achieve your greatest in God’s purpose for your life. I want you to get off the rocking horse and find a living stallion— your life’s vision.

To do this, you need to understand and put into practice principles that transcend current trends and even conventional wisdom.

In this way, your success will not be dependent on the state of the economy, what careers are currently in demand, or what the job market is like. You will not be hindered by what people think you are capable of or your initial lack of resources.

Take Your Life Out of Neutral!
You are the sum total of the choices and decisions you make every day. You can choose to stay where you are, or you can choose to pursue your dream. I challenge you to stop making excuses for why you can’t accomplish what you were born to do.

Take your life out of neutral.

You possess the power and the responsibility to determine your future and destiny. Remember, you were created to accomplish something that no one else can accomplish.

Never expect anything less than the highest thing you could go after. Don’t let people tell you, "You shouldn’t have high expectations." Dream big.

No matter how challenging it gets, don’t give up, because your vision is the key to fulfilling your life’s purp

Tuesday, November 27, 2012

Waiting and Dating Quotes-DR.Myles Munroe






“Healthy relationships should always begin at the spiritual and intellectual levels - the levels of purpose, motivation, interests, dreams,and personality.”
― Myles Munroe, Waiting and Dating


“Friendship is not a gift, but is the result of hard work.”
― Myles Munroe, Waiting and Dating


Saturday, November 17, 2012

LIVE OUT OF YOUR IMAGINATION


Tuesday, November 13, 2012

HATU PASWI KUKATA TAMAA

Tunaishi kwenye jamii ya watu walio na mitazamo tofauti juu ya maisha,wana tenda matendo tofauti,wana fikiri kitofauti,hawafanani wanapo onyesha hisia zao juu ya masuala mbali mbali ya kimaisha.

kila mmoja ana mfumo wake wa maisha,na kila siku watu wanapoendelea na maisha,hukutana na changamoto mbali mbali za kimaisha.


Tumetofautiana jinsi tunavyokabiliana na kuta tua changamoto hizo,wapo wengine wanaokata tamaa ya maisha,kwa sababu ya matatizo yanayo wakumba.

Hakuna anayependa,kukumbwa na matatizo,ukiona huna matatizo mengi,mshukuru Mungu,ujue ni neema yake ipo juu yako.Ninacho amini ni kwamba “Hatu kuumbiwa kukata tamaa” ,lakini kuna watu tayari wameshakata tamaa na maisha,na hatuwezi kuwa acha waendelee na kukata tama,ungana nami katika kuihamasisha jamii yetu,ili tuone watu wakihamasika na kuyafurahia maisha.



Kama unajifunza kitu,na unahamasika,kupitia blog hii,ni andikie ujumbe kwenye e-mail yangu(baraka1990@gmail.com),maoni yako ni ya muhimu kwangu na nina yaitaji,ili niweze kuwa katika nafasi nzuri ya kuhamasisha jamii yetu.

Monday, November 12, 2012

JOEL OSTTEEN

Watu wengi sana,wana angalia udhaifu wao,na hawa angalia uwezo wao au usahihi wao,mtu ukiangalia udhaifu wako hauta yafurahia maisha,tunapaswa kuyafirahia maisha.
Angalia uwezo ulionao,jipange na utumie uwezo wako,muda mwingi fanya vitu vinavyoendana na uwezo wako

MABADILIKO CHANYA

ili uwe mtu wa mabadiliko chanya,unapaswa kutambua mabadiliko ya kweli huanzaia ndani ya mtu,na kisha udhihirisho huanza kuonekana katika matendo yako,maneno yako,jinsi unavyoishi na jamii yako.

KUAMUA

Unaweza ukaleta mabadilko katika maisha yako,iwapo tu uta amua toka ndani yako.

HAMASA




Hii ni blog inayohusu masuala ya hamasa(Inspiration),kwa nini ninapenda kuwahamasisha watu,ni kwa sababu nina amini watu wakihamasishwa hupata hari mpya ya kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii,kupitia hamasa mtazamo wetu juu ya maisha hubadilika,yale tuliyokuwa tunaona hayawezekani,huwa tuna anza kuona yanawezekana,hali ya kukata tama huondoka ndani yetu.Hamasa hutufanya kuwa watu wenye furaha na amani

NYAMAZA

Usilie nyamaza,hilo nalo linapita.

AFRICA NI YETU

Vijana wa Africa tujitume,Africa ni yetu,tuwe suluhu ya matatizo yanayoikumba jamii.


UFANISI



Tunapaswa kutumia simu yako kwa ufanisi,ukilinganisha na uwezo wa simu yako,kama una simu yenye uwezo wa kufanya vitu vingi,hakikisha unaitumia vyema,vinginevyo utakuwa una underutilize.

MUNGU,NIGUSE TENA.


Mungu, niguse tena,ukinigusa tena,nitakuwa salama,nimejaribu bila ya wewe,sijawahi shinda,naomba uniguse tena,niguse Baba,ukinigusa wewe nitakuwa salama.

TUNA PASWA KUWA WABUNIFU


Tunapaswa kuwa wabunifu,maisha yasiyo na ubunifu ni maisha mzigo,kwanini nina sisitiza ubunifu?tunapokuwa wabunifu,tunapata suluhu ya matatizo yanayotukabili,matatizo yaliyopo yanapaswa kutafutiwa suluhu,ili maisha yasonge mbele kama inavyotakiwa.Sisi vijana tunapaswa kuwa wabunifu,ili tutatue matatizo ya jamii yetu,jamii yetu haipaswi kuyazoea matatizo,kwani hatukuumbwa ili tuishi katika matatizo,na unapaswa kutambua,matatizo yanakuja na kuondoka,wewe utabaki na kuendelea na maisha,usikate tama.

Sunday, November 11, 2012

CHOOSING TO BE POSITIVE AND HAVING A GRATEFUL ATTITUDE


UNAJIFUNZA NINI ? KUTOKA KWENYE PICHA HII

 Umeona nini kwenye hii picha?mimi naona wakina dada wa Tanzania wana paswa kujifunza kutengeneza hoja,na kuzi wasilisha mbele ya kadamnasi.


TUNAPASWA KUYAISHI MABADILIKO


Hatuna tena muda wa kulalamika,tunachopaswa kutambua,katika ulalamishi hakuna majibu,tuna paswa kutafakari juu ya mfumo mzima wa maisha yetu ya kila siku,tukitaka kuona mabadiliko chanya katika maisha yetu,tunapaswa kuyaishi mabadiliko tunayoyataka katika maisha yetu.


VIJANA WA AFRICA,TUNA MENGI YA KUJIFUNZA

Tutazame mbali zaidi,na tunuie kuwa na maono makubwa,Africa ni yetu.
Vijana wa Africa tuna mengi ya kujifunza na kuyatendea kazi,wakati wetu ndiyo huu,usikatishwe tamaa na historia ya maisha yako au maneno ambayo watu wana nena juu yako,wewe songa mbele,Mungu yupo upande wako

Wednesday, October 24, 2012

BIRTHDAY KWA AJILI YA MAENDELEO YA JAMII

Siku ya birthday yangu(6/8) nilipofikisha miaka

22,nilienda shule niliyosoma O-LEVEL,nilitoa

dazani mbili za sahani kwa staff ya walimu wa

Uyole Sekondari.Kila Kijana anapaswa,kukumbuka

alipotoka.

Wangapi kati yetu,tumewahi kutumia birthday zetu
katika kushiriki shughuli za kijamii?nadhani tunapaswa kubadili mtazamo wetu,wa kufanya sherehe kubwa kupiti kiasi katika birthday,tujifunze kuwa sehemu ya jamii.




Nikikabidhi dazani mbili za sahani,kwa makamu

mkuu wa shule ya Uyole Secondary.




Nilipata nafasi ya kuongea na wanafunzi wa kidato

cha pili.




KUJITOLEA KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII


Nikiwa na viongozi wa Mbeya youth development network,tukifanya usafi kuzunguka jengo la bohari ya hospitali ya rufaa mbeya.usafi huu ulifanyika tarehe 11/9/2012.











KUJENGA HOJA

vijana tunapaswa kuwa wajengaji wa hoja makini,tena
  hoja makini na zenye nguvu,kwa ajili ya maendeleo yetu na kwa taifa kwa ujumla








Tafakari makini.

Tafakari makini,uleta majibu mengi,katika majibu mengi,hupatikana jibu sahihi.

Saturday, August 4, 2012

TYVA FAHARI YETU, MUSTAKABALI WA TANZANIA



Kuna asasi makini,kuna vijana makini.Taifa letu ili liendelee linahitaji vijana makini,kwani siku zote taifa makini hujengwa na vijana makini.TYVA ni asasi makini ambayo inawafanya vijana wawe makini,shughuli za TYVA zimekuwa chachu ya kuwafanya vijana wajitambue,watumie vipaji vyao katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na kwa taifa kwa ujumla.TYVA imekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha na kusimamia miradi makini inayobuniwa na vijana,kwa ajili ya vijana,Walipotoka ni mbali na wamefanya mambo makubwa naya thamani sana kwa taifa letu,wanastahili pongezi

Nawapongeza waasisi wa TYVA,mlifanya uamuzi sahihi,na leo hii wote tunaona matunda ya maamuzi yenu

Nawapongeza wale wote walio wahi kuwa viongozi wa TYVA,kazi yenu ni njema sana.

Nawapongeza washauri wa TYVA,msaada wenu ni wathamani na umeleta mabadiliko chanya.

Nawapongeza viongozi wa sasa,maana naona gurudumu linasonga mbele kwa kasi nzuri.

Wanachama wa TYVA pongezi zenu,nyie mmeifanya TYVA iwe TYVA ya vijana,kwa ajili ya vijana inayoendeshwa na vijana.

Miaka 12

TYVA kufikisha miaka 12 na bado imesimama imara ni jambo jema sana,hii inaonyesha wazi kabisa ya kwamba TYVA,itaendelea vizuri sana kwa siku zinazokuja katika taifa hili.miaka 12 hii iwe changamoto kwa viongozi na wanachama,kutambua na kujipanga katika kuiendeleza asasi hii,tupo katika kipindi ambacho tunaitaji kufanya maamuzi kwa utashi wa hali ya juu,TYVA ikifanya maamuzi sahihi,tuwe na uhakika vijana makini wataongezeka na hatimaye tutaona taifa makini.

TYVA KUSINI MWA TANZANIA

TYVA imejijenga vizuri sana katika mikoa ya kaskazini,mashariki mwa Tanzania,ninajua kuna changamoto za kuifanya TYVA izidi kufungua matawi katika mikoa mingine,tunachopaswa kukifanya hapa ni kuiunga mkono TYVA ili ifike mikoani,kazi ya kuleta maendeleo ndani ya TYVA siyo kazi ya mwenyekiti tu na viongozi wengine wa asasi,bali ni jukumu la kila mmoja wetu anayeipenda na kuitakia mema TYVA,kuna kila sababu ya kuongeza nguvu mikoa ya kusini,na mwenye jukumu hilo ni wewe na mimi.

“TYVA DAY SPORTS AND BONANZA 2012”

Hii ni siku ya kipekee inayowaleta wana TYVA pamoja,hakuna sababu ya kukosa siku hii kwa vijana mliopo jijini Dar,tuwakilisheni sisi tulio nje ya Dar.siku hii iwe ni siku ya kufurahia pamoja,kupongezena kwa mafanikio ya TYVA,kufanya tathmini,na kisha kujipanga kwa miaka mingine inayofuata.

Katika viwanja vya ustawi wa jamii,michezo itulete pamoja,tunapaswa kutambua ya kwamba kupitia michezo afya zetu zinaimarika,na ndiyo maana nina kwambia huna sababu ya kukosa siku hii ya leo.

Katika Harambee,kila mmoja atambue mchango wake wa fedha unahitajika ili TYVA,isonge mbele,tuiunge mkono TYVA ili tuione Tanzania tunayoiitaji,na baada ya harambee kuisha,kutakuwa na futari ya pamoja.TYVA FAHARI YETU,MUSTAKABALI WA TANZANIA,hii iwe salamu yetu siku ya leo.