Tunaishi kwenye jamii ya watu walio na mitazamo tofauti juu ya
maisha,wana tenda matendo tofauti,wana fikiri kitofauti,hawafanani
wanapo onyesha hisia zao juu ya masuala mbali mbali ya kimaisha.
kila mmoja ana
mfumo wake wa maisha,na kila siku watu wanapoendelea na maisha,hukutana na changamoto
mbali mbali za kimaisha.
Tumetofautiana jinsi tunavyokabiliana na kuta tua
changamoto hizo,wapo wengine wanaokata tamaa ya maisha,kwa sababu ya matatizo
yanayo wakumba.
Hakuna anayependa,kukumbwa na matatizo,ukiona huna matatizo
mengi,mshukuru Mungu,ujue ni neema yake ipo juu yako.Ninacho amini ni kwamba “Hatu
kuumbiwa kukata tamaa” ,lakini kuna watu tayari wameshakata tamaa na maisha,na
hatuwezi kuwa acha waendelee na kukata tama,ungana nami katika kuihamasisha
jamii yetu,ili tuone watu wakihamasika na kuyafurahia maisha.
Kama unajifunza kitu,na unahamasika,kupitia blog hii,ni
andikie ujumbe kwenye e-mail yangu(baraka1990@gmail.com),maoni yako ni ya
muhimu kwangu na nina yaitaji,ili niweze kuwa katika nafasi nzuri ya kuhamasisha
jamii yetu.
0 maoni:
Post a Comment