Friday, July 20, 2012

USILIE,NYAMAZA




Watu wote duniani,Wanawake kwa wanaume,weupe kwa weusi na ,wanene kwa wembamba,warefu kwa wafupi,matajiri kwa maskini,wanene kwa wembamba,wasomi na wasio wasomi,wenye vyeo na wasio na vyeo,wenye umaarufu na wasio na umaarufu.Sote kwa pamoja tunakumbwa na matatizo,unaweza ukadhani jamii ya watu fulani( mfano,matajiri)haina matatizo,lakini ukichunguza kwa undani utagundua nao pia wana matatizo yao,unaweza ukadhani ya kwamba unaumwa sana,kama una uwezo wa kutembea nenda hospitali ukaone watu wanavyoumwa na wanavyoteseka usiku na mchana,wanavyoshindwa kula,nakwambia ghafla utajiona wewe huumwi.


Unaweza ukaona una tatizo la pesa,lakini tambua kuna mtu hana fedha ata hizo ulizonazo wewe na wala hajui atazipataje.Kupata hasara ni kitu kibaya,wala hakuna anayependa kupata hasara,unaweza ukapata hasara ya milioni tatu au ata kumi,lakini tambua kuna watu hapa duniani washa wahi kupata hasara ya mabilioni ya fedha,na wala hawakukata tamaa katika biashara zao,huna haja ya kukata tamaa.

Inawezekana umewahi fungwa jela miaka mitatu au ata minne,au ndugu yako yupo jela na huu ni mwaka wa sita au saba,Hebu kumbuka Mzee Madiba(Nelson Mandela) alivyokaa gerezani miaka 27,na akatoka na bado akawa raisi wa Afrika kusini.



Yawezekana masomo kwako ni magumu sana,na inachukua muda kuelewa,ya wezekana rafiki yako mpendwa amekuumiza sana,yawezekana umeonewa,umeibiwa,umenyanyaswa,umefeli,hujui la kufanya,mwaka wa tatu huu tangu umalize chuo kikuu na bado hujapata ajiri rasmi.yawezekana watu wote wanakuona wewe unamakosa mengi sana,tambua moja tu “MUNGU YUPO UPANDE WAKO,USIKATE TAMAA”

Matatizo,hayamaanishi kwamba huo ndiyo mwisho wako wa maisha.

0 maoni:

Post a Comment