Saturday, March 24, 2012

HAKUNA HAJA YA KUKATA TAMAA…

Leo hii,vijana katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na matatizo na changamoto.wapo vijana ambao wana kata tama pindi wanapokutana na matatizo na wanapoteza matumaini ya maisha yao ya baadaye.

Vijana wengi waliokumbwa na matatizo,wamefika mahali wanaona matatizo waliyonayo ni sehemu ya maisha yao,na hivyo matatizo waliyo nayo hawayaoni kama ni matatizo,bali ndivyo maisha yalivyo na wamefika mahali wanaamini binadamu wengine wanaishi maisha kama yao.

Wapo ambao wameona suluhu ya matatizo yao ni kujinyonga.wengine wamechukua hatua ya kuwa walevi wa kupindukia ili kujisahaulisha matatizo yanayowakabili,pasipo kufikiri wanajiongezea matatizo zaidi.

Kwa nini mimi?swali hili wamejiuliza vijana wengi,wanapokumbana na matatatizo mfululizo.

Matatizo mengi,tuliyonayo leo hii ni matokeo ya maamuzi,kauli na matendo yetu ya kila siku.Hatuna budi kubadili mfumo mzima wa maisha yetu,na hatua ya kwanza kubadilika ni fikra zetu,kauli zetu na matendo yetu.vijana wengi huchanganyikiwa wakati wa matatizo na hukata tama ya kufikiri zaidi na zaidi ili kupata suluhu,hakuna wakati ambapo tuna hitajika kufikiri sana kama wakati wa matatizo,na siyo kufikiri tu bali kufikiri kiundani.Na hakuna haja ya kukata tamaa,kumbuka “problems come and go, but you are here to stay”

Na; Baraka Daniel Kiranga.

+255762362413

0 maoni:

Post a Comment