Saturday, March 24, 2012

NAONA ,MACHO YASICHOWEZA KUONA.

Naona taifa linalomwamini Mungu.

Naona taifa lililobarikiwa na Mungu.

Naona taifa lenye uhuru na umoja.

Naona taifa lenye muungano madhubuti.

Naona taifa lenye uchumi imara.

Naona taifa lenye raia waliostaarabika.

Naona taifa liloshika na kuithamini elimu.

Naona watu wenye afya njema.

Naona watu wenye fikra makini.

Naona watu wanaopendana.

Naona watu wakiwawezesha watu(people empower people).

Naona watu wanaowajibika.

Naona watu wanatekelezewa haki zao.

Naona wanyonge wanakuwa na ujasiri mkuu.

Naona thamani ya pesa inakuwa kwa kasi sana.

Naona miundo mbinu inaboreshwa.

Naona ajali zinapungua.

Naona uhalifu unapungua kwenye taifa.

Naona maskini,wanakuwa matajiri halali.

Naona wanafunzi wanasoma,wanaelewa na wanafaulu.

Naona wafanya kazi wanalipwa vizuri.

Naona viwanda vinaongezeka.

Naona watu wanaomba msamaha na wanasamehewa.

Naona ubadhilifu wa pesa za umma unapungua.

Naona taifa imara.

Naona taifa imara.

Ukifuatilia na kufikiri kwa undani,juu ya mambo yanavyokwenda katika taifa.Na ukijikita zaidi katika mustakabali wa maendeleo ya taifa,utagundua kitu kimoja “wananchi wanafunguka na fursa(opportunities) zinaongezeka kwa kasi kubwa sana”.

Ninaposema wananchi wanafunguka,nina maanisha,uelewa wa wananchi juu ya masuala ya kitaifa unaongezeka,ujasiri wa kuhoji viongozi umeongezeka na unakuwa kadri siku zinavyosonga mbele.Pia tumeona watu wakihoji na kujadili Muungano.Miaka ya nyuma mambo kama hayo,yalikuwa nadra sana.Tumeona watanzania wakichambua sera za uchumi,elimu,afya,kwa lengo la kuishauri serikali iboreshe sera zake au itafute na kutengeneza sera mpya zitakazo kidhi mahitaji ya wananchi na kunufaisha taifa kwa ujumla.Achilia mbali masuala ya kitaifa,sote tumeona wabunifu katika tasnia mbalimbali,idadi ya watu wanaojiajiri inaongezeka.Kwa mifano michache tu niliyoitoa,ingawa ipo mingi.Utagundua watanzania sasa wanafunguka,nanina kubaliana nao kwa kusema “wakati muafaka ni sasa na mabadiliko ya kweli ni sasa”.

Fursa(opportunities) katika Nyanja/sekta mbalimbali zinaongezeka sana,tena kwa kasi ya ajabu.Leo hii tuna mfumo ambao unamuwezesha na kumpa nafasi mtu yeyote aliye dhamiria kujikwamua(kiuchumi,kisiasa na kijamii) kufikia ngazi ya juu ya maendeleo,ukilinganisha na hali ya maendeleo aliyokuwa nayo hapo awali.

Tatizo ni kutokuona fursa.

Tatizo lilopo,si watanzania wengi,wanajua na kutambua fursa katika mazingira yanayowazunguka.Hawajui wala kutambua fursa, kwa sababu tangu wakiwa wadogo hawakufundishwa kuzitambua fursa,lakini wengi wao ni wavivu na hawapendi kufikiri kwa undani na kufanya forecasting ya taifa miaka kumi(10),kumi na tano(15) ijayo,au wengine hawazioni fursa kwa sababu hawakutani na changamoto.Dalili mojawapo ya watu wasio na uwezo wa kuona na kuzikimbilia fursa ni “kulalamika”,ulalamishi kwao hauishi.

Nchi yetu ina fursa nyingi,wala hatuku kustahili kuendelea kupokea misaada,licha ya kuwa na fursa nyingi,ni watanzania wachache wananufaika na fursa hizo.Kwa maneno mengine,tuna watanzania wachache wanaonufaika , walio na uwezo wa kutambua fursa na kuchukua hatua na ndiyo maana wawekezaji wa kizalendo ni wachache ukilinganisha na wawekezaji wa kigeni.Kwa mantiki hiyo,wawekezaji wa kigeni wameona fursa nyingi katika taifa hili na watanzania wengi hawajaziona,na ndiyo maana tuna watanzania wengi wanaolalamika kuliko wale wanaotatua matatizo yao binafsi naya jamii kwa ujumla.Katika hali ya namna hii serikali inabebeshwa,baadhi ya lawama,ambazo haikustahili kubebeshwa.Tafakari

Katika hali hii,watu hujikita kwenye kujadili matatizo na kuyakuza(magnifying problems),kuliko kujadili kutafuta suluhisho la matatizo.Fanya uchunguzi kwenye mitandao ya kijamii,utagundua,wengi wanaelezea vizuri matatizo ya taifa hili na hata kuyakuza na kuwatia hofu au imani potofu baadhi ya watu wengine,ukichunguza zaidi,utagundua wanaotoa mitazamo iliyo na muonekano wa kutafuta au kutoa majibu ya matatizo,ni wachache sana,tena sana.Sijui kama umewahi kuligundua hilo?

Nivigumu kwa mlalamishi kuendelea

Ukiwa na watu wanaolalamika sana,uwe na uhakika,ulalamishi wao unaathiri mfumo wao wa kufikiri,kisha fikra zao zinaathiri utendaji wao shughuli za maendeleo.Kwa hiyo tukubaliane,ni vigumu kwa mlalamishi kuendelea kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Hututaki walalamikaji,tunataka watatuaji wa matatizo

Hali hii tukiendelea nayo,ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa.Kwa hiyo,hatuna budi kushugulika nayo na kuitatua hali hiyo ya ulalamishi usio na msingi.Tuna itaji vijana,waliyo na moyo wa kishujaa,wanaoona matatizo ni fursa(problems as opportunities)na siyo matatizo kama matatizo,vijana watakao fikiri zaidi na zaidi katika kutafuta majibu ya Tanzania.Hututaki walalamikaji,bali tunataka watatuaji wa matatizo,tunataka vijana walio na positive attitude katika kipindi cha matatizo.Swali langu kwako,unaona nini juu ya Tanzania.

Ili tuendelee,tunaitaji kuchagua kuendelea.Ili tuwe katika nafasi nzuri ya kuchagua kuendelea,tunatakiwa kufunguka(kujinasua) kutoka kwenye ujinga,uvivu, uwoga na tunatakiwa kuziona na kuzitambua fursa na kuzitumia ipasavyo.

Tukichagua kuendelea.Tutengeneze mipango madhubuti,ili tutakapoaanza kuendelea,iwe ni mipango inayotekelezeka na inayoleta matokeo mazuri(maendeleo ya taifa).Wataalamu wa mipango,watuongoze katika mchakato huu,wanapotuongoza watangulize maslahi ya taifa kwanza,wananchi washirikishwe,lakini pia wananchi watambua kwamba,siyo mara zote,wananchi wasubiri kushirikishwa,bali wao ndiyo wakaombe kushiriki katika kupanga mipango ya maendeleo,maendeleo hayasubiliwi,maendeleo yanafwatwa,wenye nia,wenye mipango,wenye udhubutu,watayafikia maendeleo,napenda uwe mmoja kati yao.

Mipango yote tutakayo panga,mambo yote tutakayo fanya,yawe yanafanikisha vision ya taifa.

Kwa mtazamo wangu,vision ya taifa iwe “To be economic independent nation”(kuwa taifa linalojitegemea kiuchumi).

Tuwe na uhakika,tukiwa na uchumi usiyo tegemezi,tuwe na uhakika tutafanya maamuzi yetu wenyewe kwa ajili ya kujiletea maendeleo yetu,pasipo kuingiliwa na mataifa mengine.

Uchumi wetu,tuufanye uwe uchumi imara.Tukiwa na uchumi imara,tutakuwa katika nafasi ya kuwa na bajeti ya taifa(national budget) inayojitesheleza na inayo tatua kero za wananchi,kama vile upatikanaji wa uhakika wa nishati ya umeme,upatikanaji wa elimu bora na inayowaandaa vijana kuwa wa tatuaji wa matatizo yao na ya jamii zao.

Baraka,tunafanyaje kuwa na uchumi imara?ili tuwe na uchumi imara,kwanza tunapaswa kuwa na sera nzuri za uchumi,zinazotekelezeka na zilizojaa nia ya dhati ya kuleta maendeleo,na kisha kujenga uchumi imara.

Pili,tuwe na viongozi na watendaji wazuri , wenye utashi katika kutekeleza sera hizo katika sekta mbalimbali.Kama tukikosa viongozi na watendaji makini na wenye utashi,ata kama tukiwa na sera nzuri kiasi chochote kile,hatutaweza kuendelea.Tunaitaji viongozi makini.Taifa makini hujengwa na watu makini wenye fikra makini.

Tukiwa na uchumi imara,maovu yatapungua

Mara nyingi,tunawaona watu wakitenda maovu na mabaya yaliyojaa ubaya haswa,tukidhani kwamba hawana maadili.Kutokuwa na maadili hiyo ni sababu moja tu,lakini nikwambie wengi wao wanafanya hayo maovu na mabaya kwa dhamira(makusudi)ya kutaka kutafuta fedha,ili iwatatulie matatizo yanayowakabili,wanafanya hivyo kwasababu wanatambua mshahara wanaopata,hauendani na kupanda kwa gharama za maisha,wanachofanya ni kutafuta njia mbadala(rushwa)ya kujikwamua na kumudu kupanda kwa gharama za maisha,zinavyopanda kadri miaka inavyosonga mbele.

Sote tuna tambua,anayelipwa mshahara mzuri,ana nafasi ndogo (small chance)ya kushawishika kupokea rushwa .Lakini anayepata mshara mdogo usioendana na kupanda kwa gharama za maisha,anashawishika kirahisi kushiriki vitendo vya rushwa,akigundulika kwamba kashiriki katika rushwa,walio wengi wataona,kilichompelekea mtu huyo kufanya hivyo ni kukosa maadili,ilihali ni mshahara mdogo,na ndiyo maana nikajenga mantiki hii “Tukiwa na uchumi imara,maovu yatapungua”,tukiwa na uchumi imara,watendaji wa serikali na viongozi, watalipwa mishahara inayoendana na kupanda kwa gharama za maisha,kila mmoja alipwe kwa kadri ya utendaji wake wa kazi na unyeti(sensitivity) wa nafasi aliyopo inavyohusiana na usalama wa taifa(national security).Kwa mtazamo,ambao nimeujenga hapo juu,kupokea rushwa kutapungua.

Tukiwa na uchumi imara,idadi ya vibaka,majambazi,matapeli,machangudoa itapungua.Unaweza ukaniuliza,Baraka,idadi itapunguaje?jibu langu ni “Mfumo mzuri na imara wa uchumi unachangia na kuongeza upatikanaji wa ajira,hivyo tatizo la ukosefu wa ajira(unemployment)litapungua,kama siyo kuisha baada ya muda Fulani,vijana wanapaswa kutambua,kinachotoa ajira ni mfumo wa uchumi na si kingine.Taifa lenye uchumi unao kuwa,ajira nazo huongezeka.Lakini taifa lenye uchumi unaolegalega,na ajira nazo zinalegalega”.Umaskini ni mbaya sana,tena sana,tuupinge kwa vitendo,chukua hatua ya mabadiliko.

Vijana wafundishwe,na wajifunze.

Vijana wafundishwe maadili,na wao pia wenyewe wajifunze maadili,kila mmoja kwa nafasi yake mwenye,watambue ujana unathamani kubwa kuliko tunavyo fikiri,kuwa kijana ni kuwa na fikra makini,kuwa na fikra makini uwe kijana.Lakini pia vijana,wafundishwe kujifunza kutumia fedha zao wanazopata kwa umakini na utaratibu maalumu na zaidi ya yote watumie fedha zao kwenye matumizi ya lazima.mwenye fikra makini,amenielewa ninachoandika hapa.

Vijana wafundishwe mbinu za kujitengenezea uchumi wao wenyewe na wa taifa,kwa njia halali.Vijana tuwe wepesi wa kufuatilia habari za uwekezaji,huwezi ukawa muwekezaji mzuri kama si mfuatiliaji wa hali ya uchumi,si jui ni vijana wangapi wamewahi kutembelea n88 tovuti ya benki kuu ya taifa(BOT),si jui ni vijana wangapi wanaojua kwamba kuna kituo cha uwekezaji hapa nchini(Tanzania Investment Center),vijana wangapi wamewahi kusoma sera ya taifa ya maendeleo ya vijana ya mwaka 2007,hivi sisi tunajua tunakoelekea?ni hatari sana kuishi pasipo kujua unataka nini maishani.Ni kuulize swali,wewe unaitaji nini?

Tatu,tutengeneze mazingira yanayovutia uwekezaji katika sekta mbalimbali.Uwekezaji uwanufaishe wakazi wa eneo husika mahali uwekezaji unapofanyika na siyo kuwatesa na kuwanyima haki zao za msingi.Vile vile katika uwekezaji,tuwe na mikataba safi na halali.Tusibinafsishe rasilimali zetu kwa bei poa,isiyolingana na uthamani wa rasilimali zetu.Suala si uwekezaji,suala ni kuwa na uwekezaji wenye tija na manufaa kwa taifa,na siyo kwa watu wachache.

Nne,tuwe na mfumo madhubuti wa ukusanyaji wa kodi kutoka kwa wananchi wote,mashirika yote na kila sekta inayopaswa kulipa kodi.Tanzania itajengwa na watanzania.Ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye mashirika,serikali kupitia wakala wake TRA,inapaswa kusimamia kwa umakini ukusanyaji wa kodi kutoka kwenye mashirika ya wawekezaji wa kizalendo na wa kigeni.Tukikusanya kodi ya kutosha,tutapata pato zuri la kutosha,litakalo tuwezesha kuwa na bajeti ya taifa isiyo na utegemezi kutoka nje.Kamwe hatuwezi kuendelea kwa kutegemea misaada,hakuna taifa lililoendelea duniani,kwa kutegemea misaada, wala haitakuja kutokea.

Makampuni ya uchimbaji madini,yalipe kodi inayostahili,makampuni ya huduma za mawasiliano walipe kodi wanayopaswa kulipa,serikali isisubiri ipelekewe taarifa ya mapato na matumizi na makampuni ya simu,bali itume wakaguzi wa mahesabu(auditors) wakakague,wajionee uhalisia wa mabilioni yanayopatikana kwa siku,lakini kodi inalipwa kidogo.Wakati umefika sasa,kwa serikali kupitia TCRA,inunue call counter system ,tukiwa na call counter system,itawezesha serikali kutokuibiwa mapato yake,inayostahili kupata,vile vile tukiwa na call counter system hutaona wateja wa simu wakiibiwa kwa kuambiwa wamepewa dakika moja,kumbe sekunde 43 au 47(makisio).Lakini vile vile,tujiulize hivi hizi bahati nasibu za ajabu ajabu,zinazochezeshwa na makampuni ya simu,zina lengo zuri kweli na watanzania?na kama hazina lengo zuri,tufanyaje?nani tumuoji?..kwa nini TCRA imefika mahali inaruhusu baadhi ya vituo vya luninga(television stations) kuaribu maadili ya watoto na vijana,kuna vipindi vinaonyeshwa kwenye luninga,wala havikustahili kuonyeshwa?redio zilizo nyingi zimejikita kiburudani zaidi,jamani taifa hili bado maskini,tusifarijiane.Mwenye macho ameona kitu hapa.

Wananchi wanapaswa kulipa kodi,haijalishi ni kodi ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja(direct tax or indirect tax).Watu watalipa kodi kwa uaminifu,pale tu,watakapoona kodi zao wanazolipa haziibiwi na wajanja,hazitumiki vibaya,haziwanufaishi wachache.Serikali inapaswa kusoma somo la nyakati.

Wananchi hawapaswi kubebeshwa mzigo wa kodi,kwa ajili ya kufidia uzembe/makosa ya taasisi Fulani ya serikali.Wakati umefika kwa serikali kuangalia upya na kutathmini mfumo mzima wa ulipaji kodi kwenye taifa hili.

Tano,serikali inapaswa kutumia vizuri na kwa umakini kodi zilizokusanywa kutoka kwa wananchi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.Bajeti ya taifa, ijikite kwenye matumizi ya lazima na siyo ambayo hayana ulazima.

Vijana taifa la leo,siyo la kesho.

“vijana ni taifa la kesho”,kauli hii sote,tumeisikia mara nyingi,haswa tulipokuwa wadogo.Wakati umefika kwa vijana kutambua “vijana ni taifa la leo” na wanapaswa kuchukua hatua ya mabadiliko ya kubadili maisha yao,wajifunze,wawe na moyo wa udhubutu kwenye masuala ya msingi na manufaa kwa maisha yao.Tuamke vijana ,wakati wetu ndiyo huu,saa ya mabadiliko ya kweli ni sasa,dakika ya kujitambua,tunao uwezo wa kuleta maendeleo ni sasa.Hii ni sekunde ya kutambua “ujana ni fikra makini”amua kuwa na fikra makini uwe kijana.

Tukiwa na fikra makini,matendo makini,tukidhubutu,tukiwa wa wawajibikaji,tukiwa wepesi wa kujifunza mambo ya msingi naya muhimu,tusipokuwa waoga wa kuwawajibisha wanaopaswa kuwajabishwa,kwa maslahi ya taifa.Na zaidi ya yote tukimtegemea na kumwamini Mungu tutaona taifa lenye uchumi imara,tutaona taifa lililobarikiwa na Mungu.

tutaona taifa lenye uhuru na umoja.

tutaona taifa lenye muungano madhubuti.

tutaona taifa lenye uchumi imara.

tutaona taifa lenye raia waliostaarabika.

tutaona taifa liloshika na kuithamini elimu.

tutaona watu wenye afya njema.

tutaona watu wenye fikra makini.

tutaona watu wanaopendana.

tutaona watu wakiwawezesha watu(people empower people).

tutaona watu wanaowajibika.

tutaona watu wanatekelezewa haki zao.

tutaona wanyonge wanakuwa na ujasiri mkuu.

tutaona thamani ya pesa inakuwa kwa kasi sana.

tutaona miundo mbinu inaboreshwa.

tutaona ajali zinapunguwa.

tutaona uhalifu unapungua kwenye taifa.

tutaona maskini,wanakuwa matajiri halali.

tutaona wanafunzi wanasoma,wanaelewa na wanafaulu.

tutaona wafanya kazi wanalipwa vizuri.

tutaona viwanda vinaongezeka.

tutaona watu wanaomba msamaha na wanasamehewa.

tutaona ubadhilifu wa pesa za umma unapungua.

tutaona taifa imara.

Mungu ibariki Tanzania.

Mungu wabariki vijana wa Tanzania.

Na; Baraka Daniel Kiranga.

barakakiranga@yahoo.com

+255762362413.

0 maoni:

Post a Comment