Saturday, August 4, 2012

TYVA FAHARI YETU, MUSTAKABALI WA TANZANIA



Kuna asasi makini,kuna vijana makini.Taifa letu ili liendelee linahitaji vijana makini,kwani siku zote taifa makini hujengwa na vijana makini.TYVA ni asasi makini ambayo inawafanya vijana wawe makini,shughuli za TYVA zimekuwa chachu ya kuwafanya vijana wajitambue,watumie vipaji vyao katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na kwa taifa kwa ujumla.TYVA imekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha na kusimamia miradi makini inayobuniwa na vijana,kwa ajili ya vijana,Walipotoka ni mbali na wamefanya mambo makubwa naya thamani sana kwa taifa letu,wanastahili pongezi

Nawapongeza waasisi wa TYVA,mlifanya uamuzi sahihi,na leo hii wote tunaona matunda ya maamuzi yenu

Nawapongeza wale wote walio wahi kuwa viongozi wa TYVA,kazi yenu ni njema sana.

Nawapongeza washauri wa TYVA,msaada wenu ni wathamani na umeleta mabadiliko chanya.

Nawapongeza viongozi wa sasa,maana naona gurudumu linasonga mbele kwa kasi nzuri.

Wanachama wa TYVA pongezi zenu,nyie mmeifanya TYVA iwe TYVA ya vijana,kwa ajili ya vijana inayoendeshwa na vijana.

Miaka 12

TYVA kufikisha miaka 12 na bado imesimama imara ni jambo jema sana,hii inaonyesha wazi kabisa ya kwamba TYVA,itaendelea vizuri sana kwa siku zinazokuja katika taifa hili.miaka 12 hii iwe changamoto kwa viongozi na wanachama,kutambua na kujipanga katika kuiendeleza asasi hii,tupo katika kipindi ambacho tunaitaji kufanya maamuzi kwa utashi wa hali ya juu,TYVA ikifanya maamuzi sahihi,tuwe na uhakika vijana makini wataongezeka na hatimaye tutaona taifa makini.

TYVA KUSINI MWA TANZANIA

TYVA imejijenga vizuri sana katika mikoa ya kaskazini,mashariki mwa Tanzania,ninajua kuna changamoto za kuifanya TYVA izidi kufungua matawi katika mikoa mingine,tunachopaswa kukifanya hapa ni kuiunga mkono TYVA ili ifike mikoani,kazi ya kuleta maendeleo ndani ya TYVA siyo kazi ya mwenyekiti tu na viongozi wengine wa asasi,bali ni jukumu la kila mmoja wetu anayeipenda na kuitakia mema TYVA,kuna kila sababu ya kuongeza nguvu mikoa ya kusini,na mwenye jukumu hilo ni wewe na mimi.

“TYVA DAY SPORTS AND BONANZA 2012”

Hii ni siku ya kipekee inayowaleta wana TYVA pamoja,hakuna sababu ya kukosa siku hii kwa vijana mliopo jijini Dar,tuwakilisheni sisi tulio nje ya Dar.siku hii iwe ni siku ya kufurahia pamoja,kupongezena kwa mafanikio ya TYVA,kufanya tathmini,na kisha kujipanga kwa miaka mingine inayofuata.

Katika viwanja vya ustawi wa jamii,michezo itulete pamoja,tunapaswa kutambua ya kwamba kupitia michezo afya zetu zinaimarika,na ndiyo maana nina kwambia huna sababu ya kukosa siku hii ya leo.

Katika Harambee,kila mmoja atambue mchango wake wa fedha unahitajika ili TYVA,isonge mbele,tuiunge mkono TYVA ili tuione Tanzania tunayoiitaji,na baada ya harambee kuisha,kutakuwa na futari ya pamoja.TYVA FAHARI YETU,MUSTAKABALI WA TANZANIA,hii iwe salamu yetu siku ya leo.