Thursday, September 26, 2013

Set one clear goal that really excites you

And nothing makes clear focus easier than to know exactly what you want. Set one clear goal that really excites you and write it down. Keeping it in front of you helps to keep your focus and to stay at it until it’s finished. Very important.

Wednesday, September 25, 2013

KUWA SHUJAA WAKO MWENYEWE.



Huwa unaanza usiku kisha inafuata asubuhi,wakati wa usiku mtu anaweza akajikwaa kwa sababu ya kuto ona vizuri,lakini inapofika asubuhi mtu huweza kuona vizuri na kufanya shughuli zake kwa ufanisi zaidi,asubuhi mtu huwa ana nguvu zaidi,asubuhi ya kesho amua kuwa shujaa wako mwenyewe,mara nyingi sana tunapenda kuonana na baadhi ya watu fulani katika jamii yetu,tukiamini wao ni mashujaa na wana uwezo wa kitofauti,je ulisha wahi kutamani kuonana na wewe?na je ungefurahi ungeonana na wewe au ungekuwa rafiki na wewe?TAFAKARI.

TUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJITENGENEZEA FURSA ZA MAENDELEO.


Mwaka 2011,nilipata kufuatilia kwa ukaribu kuhusu mitandao ya kijamii.Nilipata muda wa kuchambua mtandao mmoja baada ya mwingine,nilipaswa kufanya hivyo ili kubaini ni nani ni gwiji kati ya mitandao hiyo.Nilipata kujua tofauti kati ya mtandao mmoja na mwingine,na kwanini mtu utumie mtandao huu na usitumie mwingine.Na mwisho wa siku nilikuja kutambua ya kwamba Facebook ndiyo ulikuwa mtandao uliotengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu,na unaotoa huduma nyingi zaidi ukifana nisha na mitadano mingine,kama twitter, linked in ,my space na mitandao mingineyo.Uchunguzi huo ulinichukua muda,takribani mwezi mmoja. Kazi hii ilikuwa ni assignment yangu kwenye somo la Business information systems,nilipaswa kutafuta kampuni moja na kuifananisha na makampuni mengine,ili nipate kujua ninani kati yao ana competitive advantage.Uchaguzi wangu ulidondokea kwenye social networks.

Matumizi ya mitandao ya kijamii yamebadili maisha ya watu wengi sana,haswa namna ya upashanaji habari.Taarifa zimekuwa zikiwafikia watu wengi sana ndani ya muda mfupi,na vyanzo vya habari vimeongezeka,ukilinganisha na miaka ya nyuma,na hii ni changamoto kwa TCRA katika kudhibiti ubora na ukweli wa habari zinazowafikia mamia ya watu.
Kuongezeka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii,ni ishara tosha ya kwamba watanzania walio na uelewa juu ya matumizi ya internet unaongezeka,ni jambo jema hilo,ingawa tunapaswa kujiuliza maswali ya msingi,je watumiaji wa internet wanatumia kwa usahihi,na je tunatumia viwango(standards) vipi kuamua ya kwamba mtu huyu anatumia kwa usahihi na huyu hatumii kwa usahihi.Hayo yote tunapaswa kutafakari na kuchukua hatua.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ni vijana na wengi wao hutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuchat,kupost picha ambazo hazina mantiki na nyingi ni picha ambazo zimekosa maadali. kitu ambacho kinawapotezea muda mwingi,na kuharibu fikra zao na kupunguza uwezo wao wa kujikita katika masuala ya msingi,matokeo yake tumekuwa na vijana wengi ambao hawajikita katika kujiletea maendeleo yao binafsi. Kuna fursa nyingi sana kwenye mitandao ya kijamii,iwapo tu mtumiaji ataamua kutumia mitandao ya kijamii kama sehemu ya kujitengenezea fursa.
Na ni wito wangu kwa vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujitengenezea fursa za maendeleo yao.Tusipoteze muda kwenye masuala ambayo si ya msingi pindi tunapokuwa internert bali tutumie muda wetu kwenye kujifunza na kudadisi masuala ya msingi yanayoweza kutufanya tuanze kujiletea maendeleo.

Makala hii imeandikwa
na Baraka Daniel Kiranga(23)
0762362413
www.barakadaniel.blogspot.com



TUNA WAJIBU WA KUBADILI FIKRA ZETU

Makosa mengi tunayoyatenda ni matokeo ya fikra zetu,aidha tunatenda pasipo kufikiri au tunafikiri sana pasipo kutenda,na mwisho wake tunabaki kwenye maisha yale yale ya kila siku na tunafika mahali tunaridhika na matatizo tuliyonayo,tukiendelea hivi hatutafika,na hata tukifika tutafika mahali pa baya,kuna haja ya kubadilika sana,na dakika ya kubadilika ni sasa.