Sunday, December 23, 2012

MWAKA 2013 NI MWAKA WA KUBADILI FIKRA ZETU

2013 ni mwaka wa kubadili fikra zetu,na kusimamia usahihi,haki na wajibu.Tunuie toka ndani yetu,kuleta mabadiliko katika taifa hili.Wakati wa kuzubaa umeisha,wakati wa kulalamika umeisha,hatuna tena muda wa kuogopa.Kama kila kijana atatambua na kutimiza wajibu wake,tuwe na uhakika tutapata jamii ya vijana wanaowajibika,wanaowajibika kwa kumfuata Mungu,wanaowajibika katika familia zao,wanaowajibika katika masuala ya maendeleo ya taifa hili.UJANA NI FIKRA MAKINI,AMUA KUWA NA FIKRA MAKINI UWE KIJANA.

Thursday, December 13, 2012

WATOTO WADOGO WAKIFIKIA UMRI KAMA WETU WA KUITWA VIJANA,WAONE NINI KATIKA TAIFA HILI?


Vijana wanakumbwa na changamoto nyingi za kimaisha,taifa letu halina mpango rasmi na mfumo unaotambulika wa kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za dunia yenye utandawazi,ubepari ulio komaa,teknolojia inayokua kila kukicha.

Matokeo yake tumekuwa na kundi kubwa la vijana waliokata tama na wasio wathubutu katika masuala ya msingi,mamia ya vijana huko vijijini wanateseka na hali ngumu ya maisha,mamia ya vijana hapa jijini Dar wameathirika na madawa ya kulevya,mamia ya vijana wamekosa kutambua nini haswa maono ya taifa hili,mamia ya vijana wamebaki wakilalamika huku na huko.Mamia ya vijana wameshindwa kutambua maana halisi ya kuwa kijana.Twaenda wapi?

Hatuwezi kuvumilia hali hiyo,tuna taka hawa watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa kuitwa vijana,waone nini katika taifa hili?waone na kusikia yale ambayo mimi na wewe tumeyaona na kuyasikia?Tunataka wapite njia tunayoipitia leo hii?

Mimi na wewe tupo hapa leo hii,ili tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa hili,hawa watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na imara,itakayowawezesha wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa ujana,kisha wakasema taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Natoa wito kwa vijana wenzangu,wenye uwezo,wenye maono na tunaolitakia mema taifa hili, kuanzisha miradi itakayogusa watoto wa Tanzania,kwa ajili ya Tanzania ya kesho,vinginevyo tutakuwa tuna twanga maji kwenye kinu.

Nina jitafakari makosa yangu ya kimpango mkakati 2012, kwa ajili ya mpango mkakati 2013, wewe je?

Mungu wabariki vijana wa Tanzania
Mungu ibariki Tanzania.

na Baraka Daniel Kiranga(22)
+255762362413
baraka1990@gmail.com