Sunday, April 20, 2014

kujishibisha maarifa Zaidi

Kadri siku zinavyokwenda,kuna haja ya kujishibisha maarafi Zaidi. Bila ya maarifa ya kutosha,utashi wa kufikiri na mikakati yenye ubunifu,ni ngumu sana kuhimili dunia yetu yenye ushindani wa hali ya juu sana.Maarifa,utashi wa kufikiri,ubunifu ni nguvu kubwa sana,kumbuka nguvu isiyo onekana ina nguvu zaidi kuliko nguvu inayo onekana.

Thursday, March 20, 2014

UWE SAUTI YAO, KAMA ANNA AIDAN ALIVYO SAUTI YAO

Mwaka juzi 13/12/2012, Niliandika Makala yenye kichwa “watoto wadogo wakifikia umri kama wetu wa kuitwa vijana,waone nini katika taifa hili?”,Makala hii inapatikana katika blog yangu,kama iliyvo ada ya blog yangu kuandika juu ya masuala ya msingi na habari za kuhamasisha(inspiration),na siyo zile habari za nani alikuwa na nani “week end” liyopita,nani alipendeza Zaidi ya mwenzeka,nadhani tunapaswa kujadili masuala ya msingi Zaidi juu ya maisha yetu sisi vijana,taifa letu bado ni maskini ingawa halikupaswa kuwa taifa maskini,hatma ya taifa hili ipo mikononi mwetu.

Moja ya maneno yaliyopo katika makala ile ni “Mimi na wewe tupo hapa leo hii,ili tulete mabadiliko yetu,ya taifa la leo na vizazi vijavyo katika taifa hili,hawa watoto wadogo,wanapaswa kuandaliwa misingi madhubuti na imara,itakayowawezesha wao kuja kuwa vijana makini, wasije wakafikia umri wa ujana,kisha wakasema taifa letu halina mpango madhubuti wa kuwa andaa vijana kukabiliana na changamoto za kimaisha.”.

Na hapo ndipo nitakapo anzia leo hii. Tarehe 14/7/2013,mida ya sa nane mchana na dakika zake,nikiwa mitaa ya posta,jijini Dar es salaam,nilikutana na rafiki yangu.anaitwa Anna Aidan,tulisalimiana naye kwa furaha,Anna ni rafiki yangu wa karibu,sote tulikuwa tunaelekea njia moja,hivyo tulipanda gari moja,hakukuwa na foleni sana siku hiyo,kwani ilikuwa ni siku ya jumapili.
Kama ilivyo ada ya marafiki wanapokutana,wata peana habari za hapa na pale na kuulizana juu ya kila mmoja juu ya maisha yake,na mipango aliyo nayo.Katika mazungumzo yetu,tulijikuta tunajadili juu ya watoto wanao ishi mitaani na wanao omba omba, katika ya jiji.
Anna alinieleza jinsi anayoumizwa na hali hiyo ya kuona watoto wadogo wakiteseka na maisha ya kuomba omba na pasipo kuijua kesho yao na hatma ya maisha yao. Alinieleza ya kwamba kuna baadhi ya watoto wanaomba omba,na kiuhalisia hawapendi kuomba.Na akatoa mawazo yake ya kwamba serikali ilipaswa iwe na kituo maalumu cha kuwatunza watoto hao na kuwapatia malezi bora.
Sio kwamba serikali ndiyo inapaswa kuwa muasisi wa kuwatunza watoto hao,bali  kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuyaishi mabadiliko anayoyataka katika jamii.wakati tuna endelea na mazungumzo yetu,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimsaidia mototo mmoja ambaye anaomba mitaa ya posta,alinieleza jinsi ambavyo amekuwa akimnunulia yule mototo chakula,na ata kuongea naye,ili apate kujua nini haswa chanzo cha yeye kuomba. Msaada wa Anna kwa huyo mototo hauishi hapo,lakini pia amefika mahali anampatia mtoto huyo fedha kwa ajili ya matibabu.
Na pindi mtoto huyo,anapopatiwa fedha,anakwenda hospitalini,na akirudi ana muonyesha Anna dawa alizopewa hospitalini.Anna ananimbia,mtoto huyo moja kwa moja inaonekana hana asili ya kuomba omba.
Kuna mamia ya watoto katika taifa letu,wanapitia maisha magumu na hakuna mtu wa kuwasikiliza,na wala hawajui nini maana ya upendo,na wanaona jamii imewatenga na wao siyo sehemu ya jamii.Kuna Ongezeko la watoto wa mitaani kadiri siku zinavyo songa mbele,na hakuna hatua madhubuti ambazo zimekuwa zikichukuliwa,na kiuhalisia hawapaswi kuitwa watoto wa mitaani,kwani mtaa haujawai kuzaa mtoto,kuna mtu kwenye jamii anakwepa wajibu wake,sitaki kuamini kabisa ya kwamba hao watoto wanakosa ndugu kabisa.

Anna,ameyaishi mabadiliko anayoyataka kuyaona katika taifa letu,na amekuwa sauti ya matumaini kwa huyo mtoto.Kuna somo la kujifunza hapa.Wewe ni nani katika jamii yetu?au unalalamika tu juu ya mambo yanavyokwenda kombo,mabadiliko hayatakuja kama wewe hutabadilika,MABADILIKO NI WEWE.

Tuesday, January 14, 2014

MUSTAKABALI WETU


Na Baraka Daniel Kiranga(23).
Dar es Salaam
Tanzania

Kuna mambo mengi sana yanayotokea katika jamii yetu,na kila jambo lina sababu yake,na maana yake pindi linapotokea katika maisha yetu.Sisi kama vijana hatuna budi kujifunza katika hayo,tujifunze kutoka makosa ya kiungozi yanayotokea leo hii,tujifunze kutoka makosa ya kiutendaji yanapotokea leo hii,tujifunze kutoka matatizo ya kimaadili yanayozikumba nchi za Afrika ya mashariki na dunia kwa ujumla. Kwa nini natoa wito wa kujifunza katika makosa ya liyofanywa na watu wengine? Jibu pekee ni kutoruhusu matatizo hayo kujitokeze tena katika miaka ijayo, kwani tutakuwa tumepata utashi wa kuyazuia yasitokee au kukabiliana nayo pindi yanapotokea.Vijana tunapaswa kutambua ni sisi ndiyo tunaoamua mustakabali wa maisha yetu.
Yanayotokea leo hii,yana ashiria nini?yana ashiria ya kwamba Afrika Mashariki ipo kwenye mpito(Transion period),kuna mahali tunatoka na kuna mahali tuna kwenda,kuna mabadiliko ya kiuchumi yana yotokea katika nchi zetu za Afrika mashariki,Kuna mabadiliko ya kisiasa na kiungozi yanayotokea,kuna mabadiliko mengi yanatokea,katika hayo mabadiliko hatuna budi kujifunza na kutafakari kwa undani ili tujue nini maana ya mabadiliko hayo,na lipi tufanye kwa ajili ya mustakabali wa maisha yetu yajayo na vizazi vijavyo.
Tunapojifunza na kutafakari tuna kuwa katika nafasi nzuri ya kujipanga kimkakati kwa ajili ya kushughulika na matatizo sugu na masuala muhimu katika maendeleo ya watu wa ukanda wa Afrika mashariki,na tunapo anza kuongelea maendeleo ya watu,tunaongelea elimu yao,afya zao,miundo mbinu wanayotumia kila siku katika shughuli zao za maendeleo.
Sisi vijana leo tunajifunza yapi?Tungejibu vipi swali hilo kama tungeulizwa,au kila mmoja angekuwa na majibu yake?Je tunajua historia ya nchi zetu kabla na baada ya uhuru?Tunafahamu nini kuhusu uchumi wetu?nini haswa tuna itaji katika maisha yetu?
Kama kweli tuna taka uchumi wa nchi zetu ukue na kuwa uchumi imara,hatuna budi kujifunza Zaidi masuala ya uchumi,na kuwa wathubutu kwenye shughuli za kiuchumi na uzalishaji mali.Tukumbuke mustakabali wa Afrika Mashariki upo kwetu sisi vijana,tunapaswa kujifunza,tunapaswa kuwa wabunifu,na watendaji kwa ajili yetu na maendeleo ya nchi zetu.

Usipo wajibika wewe,nani mwingine awajibike,chukua hatua.Mwaka 2014 tunuie kujifunza na kutenda.