Naamini ushawahi kuwaza kwa namna hii “Lazima nifanye hiki,naamini nitafanikiwa tu,hapa ndo mahali pangu,waooh…huu ni wakati wangu”.Kadri dakika zilivyokuwa zinasonga mbele,ulikuwa unazidisha juhudi ili kufanikisha kile ulichokuwa unaamini utakipata,huku ukiwa na moyo wa ujasiri,furaha imetawala ndani yako kwasababu unaiona picha ya kile unachotaka kukifanya/kukipata,na zaidi ya yote ukipanga na kuhakiki mipango yote na kuiona inaenda sawa.
Kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele,shauku yako yakutaka kufanikiwa ikawa inapungua,ukafika wakati ukajigundua ule ujasiri uliokuwa nao,haupo tena.Furaha yako imetoweka,juhudi zako zinapungua kadri siku zinavyosonga mbele,Kufumba na kufumbua ukawa umekata tamaa,ile picha iliyokuwa nayo ndani ya fikra zako,hauioni tena na ata kama unaiona,basi inaonekana picha iliyofifia rangi,iliyokosa mvuto,mpaka haikuvutii wewe mwenyewe,ukikumbuka ulipotoka machozi yana kutililika,ukigeuka kushoto na kulia,wale uliotegemea watakuwa nawe katika kipindi cha matatizo,ndiyo wamekukumbia,unaona kama dunia haikutaki,hauoni pakuanzia.
Naandika makala hii kwa ajili yako,siyo siri nakupenda.Nimetoa muda wangu kukuandikia wewe,unajua kwa nini nakuandikia wewe?kwa sababu wewe ni kijana,bado una nguvu,bado una safari ndefu ya maisha,taifa linakuitaji,una akili nzuri sana,na wewe ni wa pekee,ukitaka uamini kwamba wewe ni wa pekee hebu angalia kiganja chako cha mkono,kisha angalia kidole gumba utaona kuna mistari mingi midogo midogo ilyojipanga vizuri sana,hiyo inaitwa finger print,dunia nzima hakuna anayefanana finger print na wewe.Uchunguzi wa kisayansi unaonyesha hakuna binadamu wanaofanana finger print,hiyo ni ishara tosha kuonyesha ya kwamba wewe ni wa pekee,na zaidi ya yote wewe ni wa thamani,thamani yako ni kubwa sana.Thamani yako haiwezi kulingana na kitu chochote hapa duniani.Tambua wewe ni wa thamani sana na Mungu anakupenda sana.
Mimi ni mwanafunzi,ninasoma shahada ya teknolojia ya mawasiliano(IT),chuo cha usimamizi wa fedha(IFM).ungekuja kunitembelea chuoni,wakati nimemaliza vipindi,ningefurahi sana,nikiwa katika hali ya furaha ningejiuliza,nina enda kukaa wapi na huyu mgeni wangu maalumu na wathamani.Takribani mita 150 kutoka IFM kuna hoteli ya Kilimanjaro,ni hoteli ya kifahari sana,lakini uwezo wa kukupeleka huko mimi sina..du wapi sasa,wazo jingine linakuja.. “mpeleke kantini” jingine nalo hilo “kantini kuna watu wengi,hatutakaa kwa utulivu na tuka ongea mambo yetu”……du wapi jamani?.Gafla wazo sahihi linakuja kwa wakati sahihi,yaani kama vile ulikuwa safari ndefu,umepigwa na jua kali,kiu kimekubana,unafika nyumbani unahamu na maji ya kunywa ya baridi,japo ukate kiu,ndivyo hili wazo la sasa lilivyokata kiu ya swali langu “nakupeleka wapi”..na jibu lake ni “Nakupeleka jumba la makumbusho ya taifa(national museum)”.
Huku nikitabasamu nina kwambia rafiki,hebu twende jumba la makumbusho,tukaone historia ya taifa letu,twende tukafahamu mababu zetu wa zamani walipotoka,na mchango wao kwa taifa hili.Kutoka hapa IFM mpaka jumba la makumbusho ni takribani dakika 3.
Baada ya kufika,bila shaka tutapokewa na wahudumu wa Makumbusho,kama ilivyo kawaida yetu,sisi watanzania,salamu kwanza,kisha baada ya hapo tutafanya malipo,na sisi japo tuchangie pato la taifa ilihali bado wanafunzi.Mwanafunzi huwa analipa 1500.Kwa hiyo tutalipa 3000,ninatoa mfukoni na ku mkabidhi mhudumu,kisha anatuonyesha njia tuna yopaswa kuifuata,ili tufike kule tunakotaka.
Tuna ona gari la kwanza kutumiwa na Nyerere,gari la pili kutumiwa na Nyerere.Tunasonga mbele kidogo tuna anza kuona utamaduni wa mtanzania na historia yake,maswaibu aliyopitia ya kuteswa na mkoloni,tunao picha za mashujaa wa Tanzania walio pigania uhuru na kujenga msingi wa taifa letu.Ndani ya muda mfupi,tuna anza kuielewa Tanzania ilitoka wapi,wakina nani wali itoa huko ilipokuwa na kuifanya tanzania kuwa ya watanzania.
kwa shauku kubwa,iliyo ambatana na furaha unajikuta unasema “hawa waliopita wamefanya makubwa sana,natamani ningekuwa wao”….ninacheka kidogo,kisha ninajibu “huwezi kuwa kama wao,wewe siyo wao.wewe ni wewe”..bila shaka utasema “baraka,mbona unanikatisha tamaa”..nitakujibu “hapana sikukatishi tamaa,wala sipendi kuwakatisha tamaa vijana wenzangu,na ningekuwa na lengo hilo,ni singekuleta hapa,nimekuleta ujifunze na mimi pia nijifunze”.
Baada ya hapo,utaniambia una maanisha nini?.Namaanisha ya kwamba kila generation inawajibu wake na kila kijana ndani ya generation husika,anawajibu wake wa kutimiza.Hii ina maana,hakuna generations zilizowahi kuwa na majukumu yanayo fanana.Ni kama vile mbio za kupokezana vijiti,generation moja ikimaliza wajibu wake,pale inapoishia,wengine wanaanza(new generation).Na ndiyo maana nika kwambia “wao ni wao na wewe ni wewe”.Sasa unachopaswa kufahamu ni wajibu wako,na jinsi gani utautimiza kwa manufaa yako na kwa taifa kwa ujumla,wala haupaswi kukata tama,kila kitu kinawezekana.Yote yanawezekana kwake yeye aaminiye.
Nina poendelea kuongea na wewe.Zile fikra za wewe kushindwa kutimiza au kufikia ndoto uliyowahi kuwa nayo zina kurudia,na zinakufanya upate hisia mbaya,usizozipenda.Bila shaka uta nisimulia na mimi bila ya iyana,nitatega sikio vizuri kweli ni kusikie uliyopitia ulipokuwa unaelekea kuitimiza ndoto yako,utanieleza changamoto ulizopitia.Utahema kwa nguvu kisha utasema “hivyo ndivyo ndoto yangu ilivyokufa,kiukweli iliniuma sana”.Nitakuangalia,kwa kutumia mikono yangu nitashika mikono yako,kisha nitakwambia “ndoto yako haikufa,bali ili lala,na sasa ndiyo wakati wake wa kuamka na mikono hii niliyoishika itatenda makuu katika taifa hili”.
Mamia ya vijana sehemu mbali mbali,hapa nchini wamekata tama na maisha.Wamepoteza dira,pasipo kujua kwamba wamepoteza dira.Wapo katika safari ambayo hawajui wanaelekea wapi,Hii ni hatari sana.
Vijana wamekata tamaa ya kufikia ndoto zao,walizokuwa nazo tangu wakiwa watoto.Kuna baadhi ya watu wamewakatisha tamaa au wamekatishwa tamaa na matatizo na changamoto za maisha,wengine hawajui ni sababu gani iliyo wafanya wakate tamaa na kila wakitaka kujinasua katika nyavu za kukataa tamaa wanajikuta ndiyo wanajifunga zaidi na zaidi.
Kuna kitu kimoja ambacho naamini.Vijana wakitiwa moyo,wakionyeshwa njia wanayopaswa kuifuata,wakiujua ukweli,kamwe hawatakata tamaa ya maisha,utawaona wale waliokuwa hawawezi sasa wanaweza,utaona ndoto zinatimia.Vijana wana weza na wana uwezo.
Ngoja nikuonyeshe baadhi ya sababu zinavowafanya vijana,wakate tamaa ya kufikia malengo yao na ndoto zao.Lakini pia nitatoa na njia za kuzuia sababu hizo ili kijana asije akajikuta anakata tamaa.Vijana hatupaswi kukata tamaa.
· Vijana wengi,huwashirikisha au kuomba ushauri kwa watu,ambao wahajafanikiwa katika maisha.Ukitaka mafanikio makubwa,omba ushauri kwa watu waliofanikiwa.Kamwe hauwezi ukachuma chungwa kwenye mgomba.
· Vijana wengi hawaandiki vision zao.Watu waliofanikiwa zaidi duniani,ni wale ambao wakipata wazo,huliandika katika vitabu vyao vya kumbukumbu(Dairy).Kulikuwa na mahafali ya wanafunzi wa masters katika chuo kikuu cha Harvard ,wanafunzi wakaulizwa “wangapi,wanajua mahali malengo yao yalipoandikwa?”ni asilimia tano tu ya wanafunzi wote ndiyo waliokuwa wameandika.Baada ya miaka 10 kupita,ikagundulika ni aslilimia 3 kati ya ile asilimia 5 ndiyo waliyofikia malengo yao waliyokuwa wameyaandika.Nataka ni kuonyeshe umuhimu wa kuandika kile unachotaka kukifanya.
· Vijana wengi,hawajui wanataka nini katika maisha yao.Faida ya kijana kujua anachokitaka maishani ni,kujua lipi analopaswa kufanya ili afikie ndoto yake na lipi hapaswi kulifanya ili lisije lika mfanya ashindwe kufikia malengo aliyojiwekea.Wewe unataka nini katika maisha yako?
· Vijana wengi, ni wavivu wa kusoma vitabu,achilia mbali vitabu vya darasani.Kijana anapaswa kuwa msomaji wa vitabu,haswa vitabu vya inspiration,leadership, na vingine vyenye masuala ya msingi.Wewe mara ya mwisho,ulisoma kitabu lini?amua kubadilika,mabadiliko yako na kwa faida yako mwenyewe,utakapo badilika utakuwa katika nafasi nzuri ya kufikia malengo yako.
· Vijana wengi wanafanya vitu,kwa sabababu wengi wana vifanya ata kama havistahili kufanyika,vibaya,vimekosa maadili.Tambua kwamba wewe si “wengine” bali “wewe ni wewe”.usifanye kitu kwa sababu wengine wanafanya,fanya kitu kwa sababu unapaswa kufanya na kwa namna moja au nyingine unachofanya kina sukuma mbele gurudumu la maendeleo yako.
· Vijana wengi,hawatumii rasilimali ya muda vizuri,tunapaswa kutambua muda huwa haungojei mtu.Anayejua vitu vingi kukuzidi ujue alijifunza kabla yako,kwa lugha nyepesi ali itumia muda vizuri, kabla wewe hujatumia muda vizuri.Nuwia toka moyoni kuwa watofauti.
· Vijana wengi siyo wathubutu kwenye masuala ya msingi naya maendeleo (to take risk, for gaining benefits).Tambua maamuzi makubwa hayawi makubwa mpaka yanapowekwa kwenye vitendo.
Nimalizie kwa kusema,yawezekana umekatishwa tamaa juu ya kile ulichokuwa una amini unakiweza.Tambua wewe siyo wa kwanza kufanyiwa hivyo,usiwachukie wanaokukatisha tamaa,wasamehe.Kuna wengi walikatishwa tamaa,lakini hawakuruhusu nafsi zao zikubali kukata tamaa,mtu pekee anayeweza kukukatisha tamaa ni wewe mwenyewe unajikatisha tamaa kwa kuruhusu nafsi yako kukata tama.Kwa mantiki hiyo watu hawawezi kutukatisha tama,bali sisi wenyewe na fikra zetu ndiyo tunaweza kujikatisha tamaa.Hakuna haja ya kujikatisha tamaa,tusikate tamaa vijana,Kwani nani amekwambi haiwezekani?usimsikie huyo.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu wabariki vijana wa Tanzania.
Na; Baraka Daniel Kiranga.
barakakiranga@yahoo.com
+255762362413.
Makala hii ni moja kati ya makala zinazoandikwa na Baraka(miaka 21),ndoto yake nikuona vijana wa Tanzania,wakitumia uwezo wao(potentials, spiritual gifts, talents)walizopewa na Mungu,kwa manufaa yao wenyewe na kwa taifa zima na kuona Tanzania yenye mafanikio ifikapo 2040.( Baraka’s vision, is to see inspired great thinkers generation by 2040 in all corners of Tanzania, he wants to see every Tanzanian learn at least one inspiration book by 2040,when they will be inspired, they will inspire and we will have inspired Tanzania).Muunge mkono,kwa kuamua kusoma kitabu(inspiration book) walau kimoja,na tuma makala hii kwa rafiki yako.
0 maoni:
Post a Comment